Quantcast
Channel: iphone – AutomobileHeat
Viewing all 553 articles
Browse latest View live

Haya ndio maneno ya H. Baba kuhusu video mpya ya Ali kiba ‘Chekecha’

$
0
0

Muimbaji Hamis Baba aka H Baba  leo ameamua kuandika kwenye ukurasa wake Instagram kuhusu video mpya ya Ali Kiba iitwayo Chekecha iliyochezwa kama ‘Exclusive’  June 29 kwenye kituo cha luninga maarufu Trace Tv ya Ufaransa. Ujumbe huo unasomeka hivi; ‘ #KIUKWELI WEE JAMAA@officialalikiba UMENIFURAHISHA SANA KWENYE HII #VIDEO KAMA NILIOTA VILE #UMEITENDEA HAKI WIMBO HUU WA #CHEKETUA PIA UMECHEZA VIZURI SANA NAUFUNDI WASAUTI SASA NIMENJOY SANA KUITAZAMA NARUDIA RUDIA TUU#SALUTE KIBA #NAONGEA KAMA#MWANAMUZIKI MWENZAKO #salute#KINGKIBA HUU WIMBO UMEUTENDEA HAKI SANA @VIDEO HATARIIII#NILICHOPENDA KWENYE HII VIDEO#LOCATION ZAKE TAMU SANA#UTAZANI SIO MAREKANI KAMA KINO AU MIGO #UVAAJI ULIOVAA UNAENDANA NA #CHEKETUA LILE BEAT LAKO NANGUO NIMEPENDA#UNAJUA NINI UNAFANYA #HONGERAZAKO #WAHUSIKA WALIOMO NDANI YA VIDEO #KIAFRIKA ZAIDI#HONGERAA SAAAANA #SINA TEAM YOYOTE HUMU NDANI ILA #KIBA ANAJUA TUACHE MASIHAraaaa MWANAMUZIKI kumkubhali mwenzio inaruhusiwa SIO KIFUNGO CHA MIAKA#30 JERA kama wenzangu wanavyoogopa #hii video nikaliiiiiiiiiiiii#wimbo mkaliiiiiiiiiiiiiiiiii FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat


Msamibaby Yala yala

$
0
0

FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Tano, 2015/ 2016

$
0
0

OWM-TAMISEMI inawatangazia majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi kwa mwaka 2015.Wanafunzi waliochaguliwa ni kutoka shule za Serikali na zisizo za Serikali. Jumla ya wanafunzi 55,003 wakiwemo wasichana 23,303 na wavulana31,700 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi.   Kati ya wanafunzi waliochaguliwa 29,744 wakiwemo wasichana 11,450 nawavulana 18,294 sawa na asilimia 54.08 watajiunga na masomo ya Sayansina Hisabati; na wanafunzi 25,259 wakiwemo wasichana 11,853 nawavulana 13,406 sawa na asilimia 45.92 wamechaguliwa kusoma masomoya Sanaa na Biashara. Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano mwaka 2015 wataanza muhula wa kwanza tarehe 18 Julai, 2015 na hakutakuwa nafursa ya mabadiliko yoyote ya shule.    Wanafunzi wote wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangwa kwa wakati. Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti kwa zaidi ya siku 14 kuanzia tarehe ya mwisho yakuripoti, nafasi yake itachukuliwa na mwanafunzi mwingine aliyekosa nafasi. Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano naVyuo vya Ufundi mwaka 2015 inapatikana kwenye tovuti ya OWMTAMISEMI ya www.pmoralg.go.tz Imetolewa na Katibu Mkuu, FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Mbunge Aiomba Serikali Ipige Marufuku Pombe za Kienyeji na Za Viwandani ( Bia)

$
0
0

MBUNGE wa Mji Mkongwe, Ibrahim Sanya (CUF), ameitaka Serikali kupiga marufuku unywaji wa pombe kwa kuwa ni kichocheo cha maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU). Akiuliza swali bungeni jana, Sanya alisema ni wakati mwafaka kwa Serikali kupiga marufuku uuzwaji wa pombe hizo zikiwemo za kienyeji na pombe za viwandani.   “Kama hilo haliwezekani basi katika bajeti ijayo iongeze tozo pombe kwa asilimia 100 ili fedha zitakazopatikana ziende zikasaidie waathirika wa Ukimwi au miradi ya REA (Mradi wa Umeme Vijijini),” alisema Sanya.   Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Stephen Kebwe, alisema Serikali imepiga marufuku unywaji wa pombe haramu.   “Vile vile tunapiga marufuku unywaji wa pombe kupita kiasi, unywaji wa pombe kupita kiasi haukubaliki, unywaji wa bia sio kunywa kreti zima.   “Kwa jinsi tulivyoumbwa binadamu tuna uwezo wa kunywa bia moja kwa kila saa moja, hata hivyo kimaumbile kwa mwanamke anaruhusiwa kunywa angalau bia moja hadi tatu kwa saa 24 na mwanaume anatakiwa kunywa bia tatu hadi nne kwa saa 24,” alisema.   Awali akijibu swali la msingi la Sanya, Dk. Kebwe alisema Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imetengeneza miongozo maalumu kwa ajili ya kuwasaidia watumishi wa afya kutoa ushauri kuhusu lishe bora kwa waathirika wa VVU wanaotumia dawa za kupunguza makali ya VVU.   “Ushauri huo ni pamoja na aina ya vyakula vinavyomfaa mtumiaji wa dawa ambavyo vinapatikana kwenye jamii yake.   “Pia waathirika wa VVU wote wanaotumia dawa za kupunguza makali ya virusi wanafanyiwa uchunguzi mara kwa mara kubaini hali yao ya lishe na kupewa ushauri au matibabu stahiki ikiwa ni pamoja na virutubisho kama vile vitamin, madini na chakula na dawa,” alisema Dk. Kebwe.   Katika swali lake Dk. Kebwe alitaka kujua Serikali inawasaidiaje waathirika wa VVU wanaotumia dawa za kupunguza makali ya VVU kupata lishe bora FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Membe alonga tuhuma za mabilioni ya Libya

$
0
0

Dar es Salaam . Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ameamua kutoa ufafanuzi wa sakata la mabilioni kutoka Libya ambayo amekuwa akihusishwa nayo, akieleza kuwa fedha zote zilizotolewa kwa amri ya mahakama ni mkopo na hazikuchotwa kama ilivyokuwa kwenye kashfa za Epa au Escrow. Membe amekuwa akihusishwa na fedha hizo, Dola 20 milioni za Marekani (sawa na Sh40 bilioni) ambazo zilikuwa zimehifadhiwa katika akaunti ya Libya No.004-200-0002216-01 iliyokuwa Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB). Kwa mujibu wa waraka alioutoa jana kwa vyombo vya habari kuhusu fedha hizo, Membe alisema Serikali ya Libya na Tanzania zilitia sahihi mkataba wa nyongeza (Addendum to the Dept Swap Agreement) ambao ulizungumzia, pamoja na mambo mengine, matumizi ya fedha hizo. Mkataba huo wa nyongeza unatamka katika kifungu No.4.02, kwamba, fedha hizo zikopeshwe kwa mwekezaji aliyeteuliwa na Libya, ambaye ni kampuni ya Meis Industries Limited kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa kiwanda cha Saruji mkoani Lindi. “Ni mkopo uliotolewa kwa Kampuni ya Meis kwa mujibu wa Mkataba wa Makubaliano (Investment Agreement) wenye masharti ya kibenki. Na Masharti hayo ya kibenki yanamtaka mwekezaji kuweka dhamana, kulipia riba, kuwekewa muda wa kurudisha mkopo, na anawekewa hatua za kuchukuliwa endapo mwekezaji huyo atashindwa kulipa mkopo,” anaeleza Membe. “Kwa lugha nyingine, kampuni ya Meis ikishindwa kulipa mkopo huo, itafilisiwa mali zake na TIB itarudishiwa fedha zake. Iacheni benki ifanye kazi yake. Mkopo unageukaje kuwa ufisadi?” Membe alisema yeye hana kampuni hapa nchini, hana ubia na kampuni yoyote, pia hana hisa katika kampuni ya Meis na hajafaidika na mkopo huo ambao unasimamiwa na TIB. “Ndiyo maana uvumi kuwa nahusika na ufisadi wa mabilioni ya Libya hauna mashiko kabisa. Baadhi ya wanasiasa wenzangu wanajua ukweli wote huu, lakini kwa makusudi wanaamua kuwafanya watu waamini,” anasema Membe kwenye waraka huo. Anasema ujenzi wa kiwanda cha saruji cha Lindi unaendelea vizuri na mitambo yote inayotakiwa katika ujenzi huo imeshawasili. “Asilimia 45 ya ujenzi wa kiwanda hicho umekamilika na ni mategemeo ya kampuni ya Meis kuwa kiwanda hicho kitakamilika ifikapo Desemba mwaka huu wa 2015,” anasema. Alisema kumbukumbu zinaonyesha mambo mawili, kwamba, kabla ya Serikali ya Libya kutia sahihi nyongeza hiyo ya mkataba iliyotaka fedha zikopeshwe kwa Meis, upembuzi yakinifu wa mradi husika ulifanywa na Libya kupitia vyombo vyake, walishajiridhisha juu ya ubora wa mradi huo. Pili alisema baada ya kutia sahihi nyongeza ya mkataba, serikali ya Libya kupitia ubalozi wake hapa nchini iliendelea kusisitiza kwa maandishi kwamba Serikali ya Tanzania iharakishe mchakato wa kuwezesha fedha hizo zikopeshwe kwa mwekezaji waliyemteua ili mradi huo muhimu usiendelee kuchelewa, na pia fedha ziingie katika mzunguko kwa manufaa ya Watanzania. “Katika kutekeleza mikataba hii miwili, yaani na kwa kuzingatia umuhimu ambao Serikali ya Libya iliuonyesha, Serikali ya Tanzania kupitia watalaamu wake wa Wizara ya Fedha, TIB, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu na Meis, walikutana chini ya usimamizi wa Wizara ya Fedha na kuandaa hadidu za rejea ambazo zilisababisha kutengenezwa kwa mkataba wa uwekezaji kati ya serikali ya Tanzania, TIB, Serikali ya Libya na Mwekezaji,” alisema. “Serikali ya Tanzania, TIB na mwekezaji walitia sahihi mkataba huu na kuupeleka Libya ili serikali ipate kuweka sahihi, lakini kwa sababu ambazo hazikufahamika, serikali ya Libya haikutia sahihi mkataba huo.” Kutokana na hilo, Membe alisema Septemba 13, 2010 mwekezaji alifungua shauri la madai No. 124/2010 Mahakama Kuu ya Tanzania, dhidi ya Libya, akiiomba Mahakama Kuu itoe tamko kwamba kitendo cha Libya kukataa kutia sahihi mkataba huo hakikuwa cha haki na kwamba mahakama itoe amri kwamba fedha hizo zitolewe kwa mwekezaji ili kutekeleza mradi uliokusudiwa. “Kumbukumbu zinaonyesha kwamba wito wa mahakama (summons) ulipelekwa ubalozi wa Libya, lakini hapakuwa na majibu wala mwakilishi aliyekuja mahakamani,” alisema. Alisema Mahakama Kuu, kwa kufuata taratibu zake, iliendelea kusikiliza shauri na kutoa amri kama ambavyo mahakama yenyewe ilijiridhisha. Amri ya mahakama, pamoja na mambo mengine, iliagiza kwamba fedha hizo zitolewe kwa mwekezaji ili kutekeleza mradi husika. Alisema TIB, AG walipinga hilo lisitekelezwe lakini mwisho wa yote maamuzi ya Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa katika mchakato mzima yakawa kwamba Meis ilikuwa na haki ya kupewa fedha za mradi wa kiwanda hicho cha saruji kama ilivyoanishwa katika mkataba kati ya Serikali na Libya. “Ni dhahiri kwamba, mgogoro huu ulichujwa na mahakama mpaka ngazi ya juu kabisa, tena kwa nyakati tofauti na mbele ya waheshimiwa majaji wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa,” alisema Membe katika taarifa yake. “Katika Taifa linaloongozwa kikatiba, chini ya utawala wa sheria kama Tanzania, ambako Mahakama ndicho chombo kilichopewa mamlaka ya mwisho kuamua juu ya haki za raia na hata serikali, si rahisi na wala haitakuwa sahihi kwa mtu yeyote kuhoji uhalali wa mchakato huu kama ulivyoongozwa, kuelekezwa na kuamuliwa na mahakama, isipokuwa tu kama sheria inatoa mwanya mwingine kurudi mahakamani kwa mtu yeyote ambaye hajaridhika au anayetaka kuhoji maamuzi haya kwa namna yoyote. “Mahakama iliamua kwa mujibu wa sheria. Na kwa kuwa hakuna aliyeendelea kupinga kimahakama, suala hili lichukuliwe kwamba limefikia mwisho na limefungwa.” FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Wanafunzi 18,751 wakosa nafasi kidato cha tano

$
0
0

Dar es Salaam . Wanafunzi 18,751 waliofaulu mtihani wa kidato cha nne mwaka 2014, wamekosa nafasi ya kujiunga na shule za kidato cha tano kwa sababu mbalimbali ikiwamo ufinyu wa nafasi. Kati ya hao, wanafunzi 479 wamechaguliwa kujiunga na vyuo vya ufundi huku idadi ya wanafunzi wa kike waliochaguliwa kujiunga na vyuo hivyo ikiongezeka kwa asilimia 25 kutoka wanafunzi 117 mwaka 2014 mpaka kufikia wanafunzi 147 mwaka huu. “Baadhi ya wanafunzi wamekosa nafasi kutokana na umri mkubwa na baadhi ya watahiniwa wa kujitegemea wanakosa sifa za kuchaguliwa,” Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Kassim Majaliwa alisema hapa jana alipokuwa akitangaza kuchaguliwa kwa wanafunzi hao. Alisema wanafunzi 55,003 sawa na asilimia 74.5 ya wanafunzi 73,754 waliofaulu mtihani wa kidato cha nne mwaka jana ndiyo waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano. Majaliwa alisema kuna ongezeko la ufaulu la wanafunzi 918 mwaka huu, ikilinganishwa na wanafunzi 54,085 waliochaguliwa mwaka 2014 kujiunga na kidato cha tano. Alisema wanafunzi waliokosa nafasi kuingia kidato cha tano watadahiliwa na Baraza la Taifa la Ufundi (Nacte) kwenye fani mbalimbali kama vile ualimu, afya, maendeleo ya jamii na kilimo. Alisema ufaulu wa watahiniwa wa kidato cha nne mwaka 2014 kuanzia daraja la ‘distinction’ hadi ‘credit’, yaani ufaulu wa wastani (GPA) wa 5.0 hadi 1.6 ni watahiniwa 73,754 sawa na asilimia 37.4 ya wanafunzi 240,410 waliofanya mtihani huo. Alisema uchaguzi ulifanyika kwa kufuata machaguo matano ya tahasusi (combinations) yaliyojazwa na wanafunzi kwenye fomu ya uchaguzi ‘Selform.’ Alisema mfumo wa kompyuta ulitumika katika kumpanga mwanafunzi katika uchaguzi wake wa masomo na shule kwa kuanzia na chaguo la kwanza. “Kama mwanafunzi atakuwa hana sifa katika machaguo yote aliyoomba, hupangiwa chaguo la somo alilofaulu zaidi na katika shule iliyopo karibu na wilaya yake ya makazi kulingana na tahasusi na nafasi zilizopo,” alisema Majaliwa. Alisema wanafunzi 29,744 watajiunga na masomo ya sayansi na 25,259 watajiunga na masomo ya sanaa na biashara. Aliwataka wanafunzi waliochaguliwa kuripoti katika shule walizopangiwa ili kuanza muhula wa kwanza wa masomo unaotarajiwa kuanza Julai 18. “Naagiza wanafunzi wote kuripoti katika shule walizopangiwa kwa wakati. Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti kwa zaidi ya wiki mbili kuanzia tarehe ya mwisho ya kuripoti, nafasi yake itachukuliwa na mwanafunzi mwingine aliyekosa nafasi,” alisema Majaliwa ambaye pia ni Mbunge wa Ruangwa, Lindi. Aliwataka wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi wa halmashauri kuhakikisha kuwa azma ya Serikali ya kila tarafa kuwa na shule ya kidato cha tano inatekelezwa kikamilifu ili kuwezesha wanafunzi wote wanaofaulu kupata nafasi ya kuendelea na masomo. “Wadau wote wa elimu pia wahakikishe kuwa shule zote zinazoanzishwa kwa ajili ya kidato cha tano zinakuwa na mabweni kwa kuwa shule hizi ni za kitaifa na zinapokea wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali nchini,” alisema. Kutokana na kuongezeka kwa ufaulu katika masomo ya sayansi, Majaliwa alihimiza shule za kidato cha tano zinazoanzishwa kuwa na maabara ili kuongeza idadi ya wanafunzi wa tahasusi za sayansi na kukidhi mahitaji ya shule husika. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

50 Cents awadiss Diddy, Waandaaji wa BET pamoja na kituo cha TV cha Fox

$
0
0

Kumbe sio tu wasanii wa bara la Afrika waliochukizwa na uandaaji na uendeshaji mzima wa shughuli za tuzo za BET, zilizofanyika jumapili ya june 28 mwaka huu kwamba hawakuwafanyia haki wanamuzi na washiriki kutoka Afrika, bali hata Rapa 50 Cents kutoka amerika hakuridhishwa na mwenendo mzima wa uandaaji wa tuzo za BET mwaka huu. Kilichomzingua na kumchanganya zaidi ni tuzo ya Mwgizaji bora wa kiume, “Best Actor” ambayo ilikwenda kwa “star” wa series ya Empire Terrence Howard. Cents alipost Video Instagram, akieleza kushtushwa na tuzo hiyo kupewa Terrence bila hata kumtaja muigizaji Omari Hardwick aliyeigiza mara nyingi na kwa uwezo mkubwa ndani ya series hiyo. “FOX bought the whole goddamn show. How you gonna have a Best Actor Award given to Terrence Howard and not even mention Omari Hardwick?” alilalama 50 kwenye video hiyo. Katika maelezo mengine 50 alisema hakuridhishwa na kile alichokifanya P Diddy wakati akiperfom na kundi lake la Bad Boy, na kutoa maneno machafu akimdiss Diddy kwamba alifanya utumbo tu jukwaani. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Diamond Kuwasha Moto Miss Kilimanjaro

$
0
0

Tareheh 24 julai 2015 miss Kilimanjaro inatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa ”KILI HOME MOSHI”ambapo Daimond atawaburuudisha wageni watakao fika katika ukumbi huo  FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat


CHADEMA Yaibwaga CCM Mahakamani……..Matokeo ya Uchaguzi Wenyeviti 16 Yatenguliwa

$
0
0

Chama cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara imezidi kupata pigo baada ya Mahakama kutengua matokeo ya uchaguzi wa wenyeviti wa vitongoji 16 vya mji mdogo wa Mirerani, kwa maelezo kuwa ulikiuka sheria na utaratibu wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.    Hii ni mara ya pili katika kipindi cha mwezi mmoja kwa Mahakama kutengua matokeo ya uchaguzi huo ambao uliwaweka madarakani makada wa CCM.   Awali, Mei 30 Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Kiteto ilitengua matokeo ya uchaguzi wa mwenyekiti wa Kijiji cha Lobosireti kwa kukiuka sheria na utaratibu.   Chadema ilifungua kesi kadhaa mahakamani hapo kupinga kitendo cha wagombea wa CCM kupewa ushindi bila kufanya uchaguzi Desemba 14, mwaka jana.   Hukumu hiyo ya jana, inatokana na kesi zilizofunguliwa na Chadema wilayani Simanjiro kwenye kata za Endiamtu na Mirerani, wakipinga wagombea wa CCM kupewa ushindi bila kupigiwa kura kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Desemba 14 mwaka jana.   Hakimu Mkazi Mfawidhi mahakama hiyo, Elimo Massawe aliagiza kurudiwa kwa uchaguzi wa viongozi wa vitongoji vya Zaire, Kisimani, Tenki la Maji, Endiamtu, Kairo na Kazamoyo vilivyoko Kata ya Ediamtu.   Hakimu Massawe alitaja vitongoji vingine kuwa ni Sekondari, Kilimahewa, Tanesco, Kazamoyo Juu, Mji mpya, Tupendane na vitongoji vya Kata ya Mirerani ambavyo ni Kangaroo, Songambele A, Getini na Songambele B.   Katika kesi hiyo, Chadema iliwakilishwa na mawakili James Millya, Shadrack Kimomogoro na Daudi Haraka na Mahakama iliamuru walipwe Sh160 milioni za gharama za kesi hiyo ambayo ilichukua takribani miezi sita hadi kutolewa hukumu.   Katibu Mwenezi wa Chadema mkoani Manyara, Ambrose Ndege alisema Mahakama imetenda haki kwa kutoa hukumu sahihi na wanajipanga ipasavyo kuhakikisha watashinda vitongoji vyote pindi uchaguzi huo utakaporudiwa.   “Tuliwaeleza tangu awali kuwa uchaguzi ukifanyika tutawashinda saa nne asubuhi hivyo tunawasubiri uwanjani na tutaongoza Mamlaka ya Mji wa Mirerani kwani wananchi wanatukubali,” alisema Ndege.   Hata hivyo, Katibu Mwenezi wa CCM wa Kata ya Endiamtu, Mashaka Jeroro alisema wanatarajia kukata rufaa kupinga hukumu hiyo akisema wagombea wa Chadema walikosea kujaza fomu ndiyo sababu wakawekewa pingamizi. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Lowassa: "Nimechoka Kuitwa Fisadi …….Mwenye Ushahidi wa Rushwa dhidi Yangu Ajitokeze Ili Aeleze nilitoa lini, wapi na kwa nani."

$
0
0

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa jana aliwataka wanaomhusisha na ufisadi kuacha mara moja kwa sababu hakuna hata chembe ya ukweli katika tuhuma hizo. Lowassa, aliyeonekana kuzungumza kwa hisia, alisema hayo jana mara baada ya kurejesha fomu ya kuwania kuteuliwa na CCM kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25. Mbunge huyo wa Monduli alikuwa mmoja kati ya makada tisa waliorudisha fomu jana, ikiwa ni siku moja kabla ya kuisha kwa muda uliowekwa na chama hicho.    Wengine waliorejesha fomu jana ni Elidephonce Bilohe, Mwigulu Nchemba, Luhaga Mpina, Dk Hamisi Kigwangalla, Hassy Kitine, Mariki Marupu, Dk Asha Rose Migiro na Lazaro Nyalandu. Hadi sasa, tayari wanachama 32 kati ya 42 wa CCM walioomba kuteuliwa na chama hicho kugombea urais wamerudisha fomu na kazi hiyo itahitimishwa leo. Hakuna mtu ambaye amejitokeza hadharani kumtuhumu Lowassa kwa ufisadi, lakini tuhuma hizo zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii, hasa kutokana na mbunge huyo wa Monduli kujiuzulu nafasi ya Waziri Mkuu mwaka 2008 baada ya kuibuka sakata la mkataba wa ufuaji umeme wa dharura baina ya Serikali na Kampuni ya Richmond RDC ya Marekani ambayo ilionekana haina uwezo. Wakati huo, Lowassa alisema kwenye hotuba yake ya kujiuzulu kuwa amefanya uamuzi huo “ili kuonyesha dhana ya uwajibikaji, lakini kutokubaliana na utaratibu uliotumika wa kusema uongo ndani ya Bunge kwa kumsingizia mtu.” Akizungumza jana kwenye ofisi za makao makuu ya CCM, Lowassa alirudia wito wake wa kutaka wenye ushahidi wa tuhuma hizo wajitokeze hadharani. “Nataka nitumie fursa hii kuwataka wale wote ambao wamekuwa wakinituhumu kwa miaka kadhaa sasa na kunihusisha na suala zima la rushwa, nawaambia waache mara moja, kwani hakuna chembe hata ya ukweli wa maneno hayo,” alisema. “Natoa changamoto kwa yeyote mwenye ushahidi wa tuhuma hizo za kipuuzi, autoe na aeleze kwa ushahidi rushwa yoyote inayonihusu, aseme nimechukua lini, kwa nani, kwa lipi na kiasi gani?” Alisema yeye ni mwadilifu na anaposema atasimamia vita dhidi ya rushwa atafanya hivyo kwa vitendo bila kumuonea mtu na bila kumuonea haya yeyote. “Ndugu wanachama wenzangu na wananchi kwa jumla, ni lazima sasa tufike mahali tuseme imetosha. Majungu yametosha, upotoshwaji umetosha, rushwa imetosha na kwa pamoja tunaweza kukomesha haya. Tutayakomesha kwa kusimamia ukweli, uadilifu, uaminifu na kutenda kwa haki,” alisema. Alisema tuhuma hizo zimeendelea hata wakati wa kutafuta wadhamini kwa baadhi ya watu kuzieneza. “Tumefanya kazi ya kutafuta na kuomba udhamini kwa uadilifu na umakini mkubwa. Na hapa nitumie nafasi hii pia kuwashukuru makatibu na viongozi wote wa Chama katika mikoa na wilaya kwa maandalizi mazuri katika kuifanikisha zoezi hili,” alisisitiza. Alisema kuwa walifanya kazi yao vizuri kinyume kabisa cha vijimaneno vilivyoenezwa kwamba kulikuwa na matumizi ya fedha katika kuwatafuta wadhamni. “Hivi kweli, unahongaje watu zaidi ya laki nane?” alihoji. Lowassa ambaye pia ni mbunge wa Monduli, alisema tuhuma hizo zimekuwa zikitolewa na watu ambao wamekosa hoja na zinatolewa bila ushahidi wowote. Alisema akifanikiwa kushika wadhifa wa urais, ataendesha nchi kwa kufuata katiba na sheria. Kuhusu safari ya kusaka wadhamini, Lowassa aliwashukuru wana-CCM waliomdhamini na kwamba walijitokeza kwa wingi jambo ambalo limempa picha ya kuungwa mkono na kukubalika. Alisema wanachama waliojitokeza kumdhamini walifanya hivyo kwa utashi wao na bila kishawishi chochote cha fedha au fadhila nyingine yoyote. Alisema kuwa udhamini alioupata ni kielelezo cha vitendo kwamba wapo naye katika Safari ya Matumaini. “Nina matumaini na imani kubwa kwamba mtaendelea kuniunga mkono ndani ya Chamna chetu ili kwa pamoja na mshikamano ndani ya Chama niweze kuteuliwa kugombea kiti cha urais,” alisema. Lowassa alisema: “Kwa mafanikio haya ya hatua ya awali nina imani kwamba ni ishara njema kueleke hatua zilizobakia na uweza wake Mwenyezi Mungu Mungu, na kwa ushirikiano wenu kwa pamoja tutalivuka daraja ili hatimaye niwatumikie kwa utumishi uliotukuka nikiwa Rais wa Awamu ya Tano.” Aliongeza kuwa: “Nina shauku kubwa ya kuunganisha nguvu na uwezo ya kila Mtanzania katika kupambana na umasikini wa nchi hii. Umasikini wa watu wetu siyo amri ya Mwenyenzi Mungu. Nina imani kabisa kwa pamoja tunaweza kutumia rasilimali tulizo nazo kwa bidii, maarifa na ufanisi zaidi ili kutokomeza umasikini huu.” Ukumbi wa Whitehouse, jana ulijaa wana-CCM ambao walifika kushuhudia Lowassa akirudisha fomu tofauti na idadi iliyowahi kutokea kwa wagombea wengine kadhaa waliomtangulia.    Hali hiyo ilisababisha foleni kwenye Barabara ya Mtaa wa Kuu unaopita mbele ya ofisi za CCM, na kusababisha usumbufu kwa wapita njia. Lowassa alifika akiwa ameongozana na mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru na wenyeviti wa chama hicho wa mikoa kadhaa pamoja na wabunge. Wabunge hao ni Andrew Chenge (Bariadi Magharibi), Peter Serukamba (Kigoma Mjini), Diana Chilolo (Viti Maalumu), Profesa Juma Kapuya (Urambo Magharibi), Mary Chitanda (Viti Maalumu), Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk Makongoro Mahanga na Mary Mwanjelwa (Viti Maalumu). Baadhi ya wenyeviti wa CCM wa mikoa waliomsindikiza ni Jesca Sambatavangu kutoka Iringa, Ramadhan Madabida (Dar es Salaam), Khamis Mgeja (Shinyanga), Mgana Msindai (Singida) na Joseph Msukuma (Geita). FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Wanne Wahukumiwa Kunyongwa Hadi Kufa Baada Ya Kukutwa Na Hatia Ya Kumuua Albino

$
0
0

MKAZI wa Kiwira, wilayani Rungwe, Hakimu Mwakalinga ambaye aliwahi kuhukumiwa adhabu ya kunyongwa hadi kufa kwa kukutwa na hatia ya kumuua Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Rungwe, John Mwakenja, amehukumiwa adhabu hiyo kwa mara nyingine baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mlemavu wa ngozi (albino).   Mwakalinga pamoja na washitakiwa wenzake watatu walihukumiwa adhabu hiyo katika Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, baada ya kukutwa na hatia ya kumuua Henry Mwakajila (17) ambaye ni mlemavu wa ngozi (albino).   Hukumu hiyo ilitolewa jana na Jaji wa mahakama hiyo, Dk Mary Levira baada ya mahakama kuridhishwa na ushahidi wa upande wa mashitaka kwamba washtakiwa hao walitenda kosa hilo.   Washitakiwa wengine ni Asangalwisye Kanyuni maarufu kama Katiti au Mwakatoga ambaye ni mganga wa kienyeji, Gerad Kalonge na Leornda Mwakisole ambao ni wakazi wa Kiwira wilayani Rungwe.   Hata hivyo, mshitakiwa wa nne, Mawazo Figomole aliachiwa huru na mahakama hiyo baada ya ushahidi wa upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha kuwa alihusika na mauaji hayo.   Kesi hiyo ya mauaji yenye kumbukumbu namba KIW/IR/49/2008 na PI 5/2013 ni kesi ya saba ya mauaji ya albino kutolewa hukumu ambapo mpaka sasa jumla ya watuhumiwa 15 wamehukumiwa kunyongwa mpaka kufa.   Awali ilidaiwa mahakamani hapo kuwa Februari 5, mwaka 2008 kati ya saa 12:00 na saa 1:00 jioni katika kijiji cha Ilolo, kata ya Kiwira, wilayani Rungwe, washitakiwa hao walimteka kijana huyo ambaye alikuwa ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Ukukwe na kumuua.   Wakati wa mwenendo wa kesi, ilidaiwa na mashahidi wa upande wa mashtaka kwamba mshitakiwa wa kwanza Kayuni ambaye ni mganga wa jadi, alikutwa na utumbo unaodhaniwa kuwa wa binadamu na ulipopelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ulithibitika kuwa ni utumbo wa marehemu Mwakajila.   Aidha, mshitakiwa wa pili Kalonge, alikutwa na vidole vinne na mifupa 10 vyote vinavyodhaniwa kuwa vya binadamu na baada ya uchunguzi vilibainika kuwa ni viungo vya Mwakajila.   Ilidaiwa kuwa, washtakiwa Mwakisole, Figomole na Mwakalinga ndio walimteka nyara mtoto huyo na kumuua, kisha kupeleka viungo kwa mganga wa kienyeji.   Mwakalinga alihukumiwa Novemba, mwaka juzi baada ya kukutwa na hatia ya kumuua Mwakenja ambaye pia alikuwa ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wilayani humo kwa kumpiga risasi.   Ilidaiwa kuwa Mwakalinga na wenzake watatu walifanya mauaji hayo kutokana na Mwakenja kufahamu kuwa wao ndiyo walimuua Mwakajila, hivyo walimuua ili kupoteza ushahidi. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Urais 2015: UKAWA Waahidi Neema Kwa Wachimbaji

$
0
0

SERIKALI itakayoundwa na Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) imeahidi kuwapa kipaumbele wachimbaji wadogowadogo ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo katika shughuli za uchimbaji wa madini huku ikihakikisha kuwa kampuni kubwa za uwekezaji zikilipa kodi stahiki ya Serikali.   Hayo yalisemwa juzi na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahimu Lipumba, alipokuwa akiwahutubia wakazi wa Kahama katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja CDT mjini hapa.   Lipumba alisema kuwa kwa sasa Serikali imekuwa haiwajali wachimbaji wadogowadogo wa madini hususani wa madini ya dhahabu ambapo wamekuwa wakigundua maeneo yenye madini kisha baadaye huondolewa na Serikali kwa kile kinachodaiwa kuwa hawana leseni za kumiliki maeneo hayo.   Alisema kuwa wachimbaji hao wamekuwa waathirika kila wanapoibua maeneo ya mgodi kwani hutolewa badala ya Serikali kuwajengea uwezo wa uchimbaji pamoja na kuwaongezea mitaji hali ambayo ingesaidia kupunguza kukosekana kwa ajira tatizo ambalo ni kubwa kwa vijana nchini.   Aidha Lipumba aliitaka Serikali kutokuwakumbatia wawekezaji wakubwa hasa wa madini na kuwasahau wale wadogo ambao ndio chanzo cha kupatikana kwa maeneo ya uchimbaji na kuwa chanzo cha kukua kwa miji midogo katika maeneo ya uchimbaji wa madini.   Pamoja na mambo mengine Lipumba alisisitiza kwa Serikali kuwatafutia wakulima wa zao la tumbaku na pamba masoko ya uhakika yatakayoleta tija kwa wakulima na kuondokana na malalamiko yaliyopo kwa wakulima wa mazao hayo kwa sasa katika Kanda ya Ziwa.   Pia Lipumba alisema Ukawa itakapoingia madarakani haitatoa nafasi kwa kampuni kubwa kusamehewa kodi kwani kwa kufanya hivyo kunarudisha nyuma maendeleo ya taifa na kukosekana pato ambalo linaweza kuwasaidia wajasiriamali wadogo ambao hawana kipato kwa sasa. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Watuhumiwa wa EPA Waachiwa Huru.

$
0
0

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewaachia huru Kada wa CCM Rajabu Maranda na wenzake waliokuwa wanakabiliwa na kesi wizi wa Sh milioni 207 katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT).   Jopo la mahakimu watatu likiongozwa na Hakimu John Utamwa, Ignas Kitusi na Eva Nkya liliwaachia washitakiwa hao baada ya upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha mashitaka dhidi ya washitakiwa hao.   Mbali na Maranda washitakiwa wengine walioachiwa huru ni Farijala Hussein na waliokuwa wafanyakazi wa BoT, Ester Komu, Bosco Kimera na Imani Mwakosya.   Akisoma hukumu hiyo Hakimu Utamwa alisema washitakiwa waliokuwa wanakabiliwa na mashitaka manne kula njama, kughushi, kuwasilisha nyaraka za uongo BoT na wiziwa Sh milioni 207.2 wako huru kutokana na upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha mashitaka hayo bila kuacha shaka kama inavyotakiwa kisheria.   Alisema upande wa Jamhuri umeshindwa kuithibitishia mahakama jinsi Maranda na Farijala walighushi makubaliano ya kukusanya deni kati ya Kampuni ya General Marketing ya India kwenda Kampuni ya Rashas (T) ya Tanzania.   Katika hukumu hiyo iliyosomwa bila Mwakosya kuwepo mahakamani, Hakimu Utamwa alisema upande wa Jamhuri wameshindwa kumleta mpelelezi wa kesi hiyo ili aweze kuithibitishia Mahakama saini ambazo zinadaiwa kuwepo katika makubaliano hayo hivyo udhaifu huo hauwezi kuwatia washitakiwa hatiani.   Aliongeza kuwa, upande wa Jamhuri ulishindwa kuthibitisha shitaka la kughushi, kwa hiyo shitaka la kuwasilisha nyaraka za uongo litakuwa limekufa,kwa sababu wameshindwa kuonesha kweli nyaraka ni za kughushi.   Aidha alisemwa wameshindwa kuonesha ni jinsi gani fedha hizo zilihamishwa kama wanavyodai kuwa mchakato huo ulifanikiwa kwa sababu Maranda na Farijala walitumia nyaraka za kughushi.   “Hakuna shahidi aliyeweza kutoa ushahidi ukaenda sawa na hati ya mashitaka iliyofunguliwa mahakamani hapo dhidi ya washitakiwa,” alisema Hakimu Utamwa.   Nyaraka zinazodaiwa kughushiwa ni hati za makubaliano ya kuhamishiwa deni kutoka Kampuni ya General Marketing ya India kwenda Kampuni ya Rashas (T) ya nchini Tanzania, ambazo walizutumia na kuiba fedha hizo.   Baada ya Hukumu hiyo, Farijala alirudishwa rumande kwa sababu anatumikia kifungo cha miaka miwili jela alichohukumiwa katika kesi nyingine na Maranda aliachiwa lakini bado ataendelea kwenda mahakamani kwa kuwa anakabiliwa na kesi nyingine.   Ndugu na marafiki waliokuwepo katika eneo hilo la mahakama walishukuru mahakama kutoa uamuzi wa haki na kusema kweli Mungu ametenda miujiza. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Majeshi ya Misri yaua wapiganaji wa IS

$
0
0

Wapiganaji wengi wa Kiislam wa kundi la Islamic State wameripotiwa kuuawa katika mapigano makali kati ya majeshi ya usalama ya Misri na kikundi hicho katika peninsula ya Sinai, kaskazini mwa Misri. Mapigano yalidumu kwa saa kadha kuzunguka mji wa Sheikh Zuwaid, kwa serikali kupeleka ndege na helikopta za kivita. Mbali na kuuawa kwa wapiganaji wa Islamic State, wanajeshi na raia ni miongoni mwa waliopoteza maisha. Habari kutoka mjini Cairo, Majeshi maalum ya usalama ya Misri yalizingira jengo moja na kuwaua wafuasi tisa wa kikundi cha Muslim Brotherhood. Wizara ya mambo ya ndani imesema watu hao walishukiwa kupanga mfululizo wa mashambulio. Kikundi cha Muslim Brotherhood kimesema wafuasi wake tisa waliuawa kikatili na kimewataka wafuasi wake kufanya maasi dhidi ya Rais Abdel-Fattah el-Sisi. Wapiganaji wa Islamic State wamekuwa pia wakiendesha mashambulizi katika nchi za Syria na Iraq kwa lengo la kuzitawala nchi hizo. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Kahaba kwa miaka 25

$
0
0

 Brenda Myers-Powell alikua mtoto wakati alipoanza kufanya ukahaba katika miaka ya sabini. Alizaliwa eneo la Chicago, Marekani na mamake mzazi alifariki dunia akiwa na miezi sita pakee. Hapo ilimlazimu kusalia na bibi yake. Aligundua baadaye kwamba mamake alikufa kutokana na ulevi wa kupindukia.Kwa sababu bibi yake alikua mfanyikazi wa ndani ilimlazimu Brenda kujipeleka shule na kurejea nyumbani wenyewe licha ya kwamba alikua kwenye chekechea. Baadhi ya watu walimdhulumu kingono mtoto huyo wakati alipokua akitoka chekechea. Mwanamama huyu alifanya ukahaba kwa miaka 15, wakati huu wote hakuwahi kujiingiza katika mihadarati. Lakini kutokana na mazingira magumu kwenye madanguro ya ukahaba, hakuwa na budi kuanza kutumia mihadarati ili kusahau maisha aliyokua akiishi. Baadaya ya miaka 25 kama kahaba, siku moja alikutana na mteja ambaye alikua katili.Alimtupa nje ya gari lake huku likienda kwa muendo wa kasi. Brenda alipata majeraha mabaya kiasi cha kupelekwa hospitalini akiwa mahututi. Lakini madaktari waliokua wakimhudumia walimdhihaki kwamba alipata alichotaka na kumsuta kwamba alikua kahadaa mteja ndiposa akapata adhabu. Hapo wakawaita polisi kumkamata.    Lakini kwa bahati nzuri daktari mmoja alizungumza na Brenda na kumshauri afike katika kituo cha huduma ya jamii maarufu kama Genesis House. Msimamizi wa kituo hiki alikua Bi Edwina Gateley raia wa Uingereza. Ni katika kituo cha Genesis Brenda alipata maisha mapya na kuanza safari ya kupona machungu, adhabu na kero za ukahaba. Hakupata shinikizo za kuondoka hadi pale alipohakikisha maisha yake yalikua shwari. Kwa sasa Brenda anawasaidia wanawake na wasichana wanaokimbia ukahaba. Aidha alijaaliwa kuwa na familia, mume na wanawe wawili wa kike. Ana pia wajukuu. Maisha yake ni kuwafundisha soka watoto na kuhakikisha wanaishi kwa maadili mema. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat


Joule’s Law of Heating

$
0
0

We know about the heating effect of current, when it flows through a circuit due to collision between electrons and atoms of wire. But precisely how much heat is generated during current flow through a wire, on what conditions and parameters does it depend? How can we know about this? To solve this problem, Joule coined a formula which explains this phenomenon accurately. This is known as Joule’s law. This law is explained in detail afterwards. Joule’s Law of Heating The heat which is produced due to the flow of current within an electric wire, is expressed in Joules. Now the mathematical representation or explanation of Joule’s law is given in the following manner. i) The amount of heat produced in current conducting wire, is proportional to the square of the amount of current that is flowing through the circuit, when the electrical resistance of the wire and the time of current flow is constant. i.e. H ∝ i2 (When R & t are constant) ii) The amount of heat produced is proportional to the electrical resistance of the wire when the current in the circuit and the time of current flow is constant. i.e. H ∝ R (when i & t are constant) iii) Heat generated due to the flow of current is proportional to the time of current flow, when the resistance and amount of current flow is constant. i.e. H ∝ t (when i & R are constant) When these three conditions are merged, the resulting formula is like this – Here ‘H’ is the heat generated in Joules, ‘i’ is the current flowing through the circuit in ampere and ‘t’ is in seconds. When any three of these are known the other one can be equated out. Here, ‘J’ is a constant, known as Joule’s mechanical equivalent of heat. Mechanical equivalent of heat may be defined as the number of work units which, when completely converted into heat, furnishes one unit of heat. Obviously the value of J will depend on the choice of units for work and heat. It has been found that J = 4.2 joules/cal (1 joule = 107 ergs) = 1400 ft. lbs./CHU = 778 ft. lbs/B Th U It should be noted that the above values are not very accurate but are good enough for general work. Now according to Joule’s law I2Rt = work done in joules electrically when I ampere of current are maintained through a resistor of R ohms for t second. By eliminating I and R in turn in the above expression with the help of Ohm’s law , we get alternative forms as FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Ray C : Naomba kuwatangazia kuwa natafuta mchumba wa kuishi naye milele! Atoa vigezo 10 vya mume amtakaye

$
0
0

Msanii wa muziki Rehema Chalamila aka Ray C amefungua mlango kwa mwanaume yoyote anayetaka kumuoa ajitokeze ilimradi awe na vigezo 10 ambavyo ameviainisha. Kupitia ukurasa wake wa instagram Ray C ameandika: “Habari zenu wapendwa wote dunia nzima!Leo na habari nzuri sana kwenu,Naomba kuwatangazia kuwa natafuta Mchumba wa kuishi nae milele!nataka niwe nae milele na nimzalie watoto wawili wa kike na wakiume!!!! Ila naomba niwambie kabisa masharti 1.Awe mpole ili nikikasirika anibembeleze   2.Awe anapenda muvi za kihindi ili nikiwa na stress aniwekee nyimbo za kihindi maana ndio raha ya moyo wangu.   3.Asiwe muongeaji sana sababu huwa sipendi makelele.   4 Anipende na ubonge wangu huu asije akaanza kunambia baby anza mazoezi au dah baby zamani ulikuwa bomba au rudisha kiuno hapo hatutaelewana.   5.Awe ananipikia nikichoka maana navutiwa nikimuona mwanaume anapika.   6.Awe na Mimi muda wote maana na wivu sana ikiwezekana tufanye kazi ofisi moja au awe ofisi ijengwe hapo hapo nyumbani.   7.Awe mvumilivu maana nikiwa na hasira huwa naongea kwa sauti ya juu sana.   8.Asiwe na rafiki wengi,na akitaka kuonana nae na mi niwepo maana si mnajua wanaume tena wakikutana huwa wanashaurina mabaya.   9.Awe anajua nyimbo zangu zote ndio ntaamini kweli ananipenda.   10.Sharti la mwisho kabisa ambalo ni muhimu sana kwangu ni hili tuwe tunatumia simu moja na Namba moja, maana kanisani tunafundishwa kuwa ndoa maana yake tumeungana na kuwa kitu kimoja kwahiyo kama mume na mke tunalala pamoja kitanda kimoja na kuishi pamoja kwanini tusitumie simu moja!Sioni tatizo! Kama una ndugu,jamaa.kaka,rafiki yuko single basi mjulishe tangazo hili huezi jua unaeza ukashangaa nimekuwa shemeji yako au wifi yako”. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Tume Ya Uchaguzi Yatangaza Kuanza Uandikishaji BVR Dar es Salaam na Pwani

$
0
0

Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la wapiga kura kwa teknolojia ya Biometric Voters Registration (BVR) lililoahirishwa katika jiji la Dar es salaam na mkoa wa Pwani hivi karibuni sasa litafanyika kuanzia  Julai 7-20 kwa mkoa wa Pwani na Julai 16- 25 kwa jiji la Dar es salaam.  Uboreshaji wa Daftari hilo kwa jiji la Dar es salaam na Mkoa wa Pwani uliahirishwa kutokana na kuchelewa kwa vifaa vya uboreshaji kutoka mikoani ambavyo vilipelekwa ili kuongeza ufanisi kutokana na maeneo hayo kuwa na idadi kubwa ya watu wenye sifa ya kuandikishwa kuwa Wapiga Kura. Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Julius Mallaba amewataka wananchi wote wa mikoa hiyo kujitokeza kwa wingi kwenye vituo vya uandikishaji vitakavyokuwa kwenye Vijiji, Vitongoji na Mitaa ili kujiandikisha  waweze kupiga kura na kuchagua viongozi wanaowataka katika Uchaguzi Mkuu Mwezi Oktoba Mwaka huu. Amewataja watakaohusika na zoezi hili kuwa ni watu wote waliotimiza umri wa Miaka 18 na kuendelea na wale watakaotimiza Miaka 18 ifikapo mwezi Oktoba Mwaka huu. Wengine ni waliojiandikisha awali kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura la zamani ili kuhuisha taarifa zao na kupata kadi mpya za kupigia kura. Aidha Mallaba amewataja wengine wenye sifa ya kujiandikisha kuwa ni wale wote wenye sifa za kujiandikisha lakini hawajawahi kujiandikisha kwenye Daftari hilo. Amesema wale wote wenye Kadi za kupigia Kura za zamani wanatakiwa kwenda na Kadi zao ili kurahisisha uchukuaji wa taarifa zao na kadi hizo zitarudishwa NEC na watapata vitambulisho vipya.  Wananchi wanatakiwa kujiandikisha katika Vituo vilivyopo ndani ya Kata zao ili kuweza kupata fursa ya kumchagua Diwani, Mbunge na Rais. Mkurugenzi huyo ametoa wito kwa wananchi wa mikoa hiyo kuhakikisha wanajiandikisha kwani bila kufanya hivyo hawataweza kupiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu. Vituo vya kujiandikisha vitafunguliwa kila siku kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa ifikapo saa 12:00 jioni.  FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Mzee Majuto Adai Kushobokewa na Vibinti

$
0
0

 Staa mkongwe kunako filamu Bongo, Amri Athuman ‘Mzee Majuto’ amefungukia shutuma anazopewa na mashabiki wake kwa kupenda kuonekana na ‘vibinti’ kuwa wanamshobokea mwenyewe. Mzee Majuto ambaye kifani ni bingwa wa komedi amesema, kutokana na kazi yake ya uigizaji imemfanya kuzimikiwa haswa na mabinti. “Sijawahi kumshobokea binti yoyote ila wenyewe ndiyo huwa wananishobokea kutokana na uigizaji wangu,” amesema Mzee Majuto. Hivi karibuni, Mzee Majuto alidaiwa kuoa binti mdogo ambaye ni sawa na mjukuu wake mwenye umri wa miaka 18 akidai kuwa sheria ya dini inamruhusu kufunga ndoa na wake wanne. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Familia Yampa ONYO Rose Ndauka

$
0
0

Staa wa filamu Bongo, Rose Ndauka hivi karibuni amewekwa chini na familia yake na kupewa onyo kuhusu wanaume pamoja na maadili.   Kwa mujibu wa chanzo, Rose aliambiwa maneno mengi na familia yake ikimtaka ajirekebishe na haswa ajitume zaidi katika kazi zake anazofanya.   “Familia yake imeamua kumuweka chini na kumwambia mengi kuhusu maisha haswa ikimtaka ajirekebishe tabia yake kwa ujumla,” kilisema chanzo.   Rose alipotafutwa kuweka wazi juu ya hili, alifunguka; “Kila familia ina utaratibu wake, kwahiyo mimi kuwekwa na familia na kupewa onyo wala siyo suala la ajabu.” FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Viewing all 553 articles
Browse latest View live