Quantcast
Channel: iphone – AutomobileHeat
Viewing all 553 articles
Browse latest View live

Wananchi wala ubuyu kutokana na njaa-Manyoni

$
0
0

MBUNGE wa Manyoni Mashariki, Kapteni John Chiligati, amesema baadhi ya wananchi jimboni kwake wameanza kula ubuyu kutokana na kukabiliwa na tatizo la njaa. Katika swali lake bungeni jana, Mbunge huyo alitaka kujua ni lini Serikali itapeleka chakula cha msaada haraka ili kuwanusuru wananchi hao. “Lini Serikali itaanza kugawa chakula cha msaada kwa kuwa jimboni kwangu kuna uhaba wa chakula, hasa katika maeneo ya Kintiku ambapo baadhi yao wameanza kula ubuyu?” alisema Kapteni Chiligati. Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi, alisema taratibu za kuomba chakula cha msaada zinatakiwa kuanzia wilayani kwa kufanya tathmini. “Wilaya ikishafanya tathmini inatakiwa kuipeleka katika kikao cha Ushauri cha Mkoa (RCC), RCC itapeleka Ofisi ya Waziri Mkuu ambao wataleta wizarani kwetu kwa ajili ya kupeleka chakula cha msaada. Chakula kipo cha kutosha, mikoa husika inatakiwa kufanya tathmini ili ituletee watu wasije wakafa njaa,” alisema. Awali Zambi akijibu swali la msingi la Kapteni Chiligati, lililohoji iwapo serikali ipo tayari kushirikiana na wananchi wa Manyoni kupitia Halmashauri ya wilaya hiyo kuhakikisha ujenzi wa bwawa la Mbwasa unakamilika, alisema ujenzi huo utafanyika pamoja na skimu ya umwagiliaji ya Mwiboo. “Skimu ya Mwiboo haipo katika skimu 78 zinazotekelezwa kupitia Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN). Wizara kwa kushirikiana na halmashauri za wilaya zimeandaa andiko kwa ajili ya kuomba fedha kwa washirika wa maendeleo ambao maombi ya Sh milioni 400 yamewasilishwa,” alisema Zambi. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat


ACT-Wazalendo yalia na rasilimali nchi

$
0
0

 CHAMA cha ACT- Wazalendo kimesema kitaleta sera  mahususi na zenye mapinduzi kuhusu utajiri wa nchi unavyopaswa kuwa na faida kwa wananchi wake. Hayo yalisemwa na Kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe, alipokuwa akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Nkanaredi, mkoani Mtwara. “Tuna utajiri wa madini, mafuta na gesi. Hapa Mtwara ni kituo kiongozi cha harakati za wananchi kufaidi maliasili zao.  Mliumizwa katika harakati hizo muhimu sana za kuhakikisha kuwa utajiri wa nchi unatumika kwa ajili ya wananchi,” alisema. Alisema Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imetangaza miswada ya sheria ya kurekebisha sekta ya mafuta na gesi, ambapo wamepeleka miswada hiyo bungeni kwa ajili ya kujadiliwa, huku ikiwa haijawahusisha wananchi.  “Miswada hii ni miswada muhimu sana kuhusu namna utajiri wa mafuta na gesi ya nchi yetu unapaswa kusimamiwa. Serikali imepeleka miswada hii chini ya hati ya dharura. Kama kuna wadau wakubwa katika sekta ya mafuta na gesi hakuna wadau zaidi ya watu wa Mtwara na Lindi. “Miswada hii inapelekwa bungeni bila kupata maoni yenu. Haikubaliki, ACT Wazalendo inataka miswada hii iondolewe bungeni ije kwa wananchi ipate maoni na kujadiliwa na Bunge la 11 litakalopatikana baada ya uchaguzi mwaka 2015. “Muswada wa Mafuta umetungwa bila ya kuzingatia mchakato wa Katiba ya nchi. Rasimu ya Katiba imeondoa suala la mafuta na gesi kwenye orodha ya mambo ya Muungano. Sheria iliyopelekwa bungeni inatamka kuwa sheria hiyo itatumika Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar,” alisema. Zitto alisema muswada wa usimamizi wa mapato ya mafuta na gesi pia umetamka kutumika pande zote za Muungano kinyume na nia ya kuondoa masuala ya mafuta na gesi  katika orodha ya mambo ya Muungano. “Ni kichekesho na Serikali kuahidi kwa Wazanzibari kuwa mafuta na gesi si suala la Muungano halafu inatunga sheria za mafuta na gesi za kutumika Zanzibar. Miswada hii haikufikiriwa vizuri na hivyo iondolewe.” Alisema muswada wa mapato ya mafuta na gesi imeandikwa haraka haraka na umeacha kabisa kushughulikia suala la mgawo wa mapato ya mrabaha kwa maeneo yenye utajiri huo. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Mashine ya BVR Yaibiwa Jijini Mwanza, wawili watiwa mbaroni

$
0
0

Watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana, waliiba mashine moja inayotumika kwa ajili ya kuandikishia vitambulisho katika daftari la kudumu la wapiga kura (BVR) katika kata ya Kayenze wilayani Magu mkoa wa Mwanza. Akizungumza na mwandishi wetu, kamanda wa polisi wa mkoa wa Mwanza, Charles Mkumbo, amesema mashine hiyo pamoja na nyingine 13, zilienda kuchajiwa katika nyumba ya kulala wageni ya BM Lodgei, lakini asubuhi zilipofuatwa haikuweza kupatikana. Kamanda Mkumbo amesema baada ya kupata taarifa ya kuibiwa mashine hiyo, msako mkali ulifanyika ukiwamo wa kuwahoji wasimamizi wa mashine hizo. Anasema baada ya kufanyika msako mkali kwa kuweka vizuizi sehemu mbalimbali, walifanikiwa kuikuta ikiwa imetelekezwa njiani ikiwa salama bila kuharibiwa, lakini hakuna mtu aliyeweza kukamatwa. Hata hivyo, kamanda Mkumbo amesema polisi wamefanikiwa kuwashikilia watu wawili wa nyumba hiyo ya kulala wageni kwa mahojiano ili kufahamu mashine hiyo ilivyoweza kutoweka katika mazingira ya kutatanisha. Aidha, ametoa wito kwa waandikishaji kuwa makini pale wanapohifadhi mashine hizo ili zisiweze kuharibiwa ama kuibiwa na watu wengine. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

H Bridge motor control circuit using L298

$
0
0

Description : A bidirectional H bridge DC motor control circuit is shown here. The circuit is based on the IC L298 from ST Microelectronics. L298 is a dual full bridge driver that has a wide operating voltage range and can handle load currents up to 3A. The IC also features low saturation voltage and over temperature protection. In the circuit diode D1 to D4 are protection diodes. Capacitor C2 is the logic power supply filter and capacitor C2 is the supply voltage filter. The state of the motor will depend on the logic level of the pins 10, 11, 12 and it is described in the table shown below the circuit diagram. Circuit diagram of H bridge motor controller: Notes :     Do not connect a motor that consumes more than 2.5A of current.     The main power supply can be anything between 3 to 40V DC.     It is advised to fit LM298 with a proper heat sink. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Mafuriko Ya Lowassa Yatua Jijini Dar……Kingunge Amwaga Wino Hadharani Kumdhamini, WanaCCM 212,150 Wajitokeza Kumdhamini

$
0
0

WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Ngoyai Lowassa amepata udhamini wa kishindo katika mkutano uliofanyika jana katika ofisi kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kinondoni. Lowassa alipata udhamini huo baada ya wanachama kujitokeza katika ofisi za Makao Makuu ya CCM ya Wilaya ya Kinondoni, Mkwajuni, Dar, ambapo alipata zaidi ya wadhamini 212,150 huku akisema Dar imevunja rekodi ya mikoa yote ya Tanzania. Akizungumza na maelfu ya wananchi waliofika katika mkutano huo Lowassa alisema kuwa amefurahishwa na watu waliojitokeza kumdhamini kwa kishindo kikubwa na hivyo hatavunjwa moyo na maneno ya watu yanayovumishwa kuwa anawapatia fedha ili wafike kwenye mkutano wake . Lowassa aliongeza kuwa anawaomba Watanzania wampe ridhaa ya kuwa rais wao kwani atahakikisha mianya yote ya rushwa na utendaji mbovu wa kusuasua anausimamia kwa haki na weredi na ndani ya miezi sita tayari matokeo yatakuwa yameonekana. “Nawaombeni wananchi mnipeni ridhaa ya kuingia ikulu yaani nitahakikisha mianya yote ya rushwa na ufisadi nautokomeza, muyapuuze maneno na minong’ono ya watu kutaka kunichafua,” alisema. Mwanasiasa Mkongwe hapa nchini, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru akisani fomu ya udhamini mbele ya Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa ikiwa ni ishara ya kumuunga mkono mgombea huyo. Zoezi hili lilifanyika jana jioni ya Juni 27, 2015 kwenye Ofisi za CCM Wilaya ya Kinondoni, Mkwajuni Jijini Dar ambapo Lowassa alipata jumla ya Wadhamni 212, 150 na kuifanya Dar es salaam kuwa Mkoa wa kwanza kuwa na idadi kubwa ya WanaCCM waliomdhamini . FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

NCCR- Mageuzi Wasema Hawana Mpango wa Kujitoa UKAWA

$
0
0

CHAMA cha NCCR-Mageuzi kimesema hakitajitoa katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) pamoja na kuwapo kwa vikwazo vya ugawaji wa madaraka ndani ya umoja huo.   Akizungumza katika kikao cha Kamati Kuu cha chama hicho kilichoketi jana katika Hoteli ya Travertine jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia, alisema lengo la umoja huo lilikuwa ni kuunganisha nguvu ili kuwa na sauti moja ya ushirikiano.   “Yapo maneno mengi yamesemwa na waandishi, wachochezi  wanasema NCCR inataka kuvunja Ukawa, tangu lini mama akakata mkono wa mtoto wake?   “Kama kuna wenye wazo la sisi kujitoa kwenye umoja huu ni vizuri watambue kuwa hatuna  mpango huo, na hili ni azimio lililotolewa na wajumbe wa Halmashauri Kuu. Pia itambulike kuwa chama hiki ni zao la Ukawa, hivyo si jambo rahisi kujitoa,” alisema Mbatia.   Alisema Ukawa si sehemu ya kugawana madaraka na kudai kuwa umoja huo unaangalia zaidi masilahi ya wananchi.   Mbatia alisisitiza pamoja na uchochezi uliopo na changamoto ya ugawaji majimbo, wanaamini watavuka kwa kuwa lengo ni kusaidia wananchi na si vyama husika.   Alisema umoja huo umejipanga vizuri, hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi  kwakuwa wana uwezo wa kutoa rais pamoja na viongozi wengine watakaounda Serikali. Ajitosa  Sakata  la  Zanzibar Aidha Mbatia alishagazwa na hatua ya Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein kuvunja Baraza la Wawakilishi juzi bila tukio hilo kuhudhuriwa na Makamu  wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad  baada ya wabunge na wawakilishi kumkatalia kuhudhuria.   “Nimeshangaa sana rais wa Zanzibar anavunja Bunge yupo mwenyewe  bila Maalim Seif. Nini maana ya Serikali ya Umoja wa Kitafa?” alihoji Mbatia.   Alisema wanachama wa vyama vya CCM na CUF wanapaswa kutambua kuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ni makubaliano  na mali ya Wazanzibari wote na si wanasiasa pekee.   Akizungumzia kuhusu mwenendo wa uandikishaji wa daftari la wapigakura unaosimamiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kutumia mfumo wa kielektroniki (BVR), alisema hakuna dalili za daftari hilo kukamilika kwa wakati kutokana na kasi ndogo ya uandikishaji.   Alisema kutokana na hali hiyo, kuna viashiria vinavyoonyesha uchaguzi utakaofanyika Oktoba hautakuwa huru na wa haki.   “Uchaguzi hautakuwa huru na haki kwa sababu wameshindwa uandikishaji, kama leo wanasema kuna zaidi ya watu 5,000 wamejiandikisha mara mbili, wanamaanisha nini kwa wananchi?   “Tulishauri tangu mwaka jana kuhusu utaratibu wa uandikishaji na muda wa kuanza, lakini wenzetu wakawa wanabisha. Kwa hapa tulipofikia lolote likitokea  wa kulaumiwa ni Serikali ya CCM,” alisema Mbatia.   Alisema hadi sasa kuna baadhi ya mikoa ikiwamo Dar es Salaam na Pwani bado hawajaandikishwa. Pia NEC inapaswa kuwa na muda wa kuhakiki  majina ambako kutafanywa na wananchi.   Aliongeza kuwa Serikali ya awamu ya nne tangu ilipoingia madarakani mwaka 2005  imekuwa ikipoteza mvuto siku hadi siku kutokana na kutowajibika kwa ufasaha.   Alisema hadi sasa kuna mazingira ambayo mtu yeyote makini ni rahisi kuona jinsi Serikali ya CCM ilivyopoteza utashi, mvuto  na mwelekeo wa kuongoza Watanzania. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Bunge linapochemka ndio raha yetu- Lissu

$
0
0

Dodoma . Bunge la 10, ambalo linamaliza kazi yake Julai 8 kabla ya kuvunjwa siku moja baadaye, lilikuwa na mengi, lakini mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu anasema kilichowafurahisha wapinzani ni wakati chombo hicho kinapochemka kutokana na hoja zao. Mwananchi ilifanya mahojiano na Lissu, ambaye ni msemaji mkuu wa Kambi ya Upinzani, ambaye alizungumzia nyakati ambazo wapinzani walifurahia sana na masuala mengine. Swali: Bunge la 10 linamaliza muda wake, unaweza ukalielezea vipi? Lissu: Ninaweza kuliangalia kwa mitazamo tofauti, kwanza nikianza na Bunge la mwaka 1964-1965, ni Bunge la kuijenga Tanganyika kutoka katika Bunge la Kikoloni, 1965-1970, lilikuwa Bunge la Azimio la Arusha. Bunge la 1970-1975, halikuwa na kazi kubwa, lilikuwa katika maandalizi ya kutengeneza Katiba ya Tanzania. Mwaka 1975-1980 lilikuwa Bunge lililotengeneza Katiba ya sasa pamoja na kumlea mwana aliyezaliwa, CCM. Mwaka 1980-1985 lilikuwa Bunge la mageuzi na mabadiliko ya Katiba hasa katika masuala ya haki za binadamu na Muungano. Hapa sasa ndipo ilipoonekana kuwa Tanzania na Zanzibar ni moja kwa sababu mtikisiko wake ulimweka pembeni Rais Aboud Jumbe mwaka 1984. Mwaka 1985-1990 lilikuwa Bunge la vuguvugu la mageuzi na Bunge la 1990-1995 lilikuwa Bunge la kwanza la vyama vingi. Mwaka 1995-2000 hakukuwa na mabadiliko sawa na Bunge la 2000-2005. Mwaka 2005-2010 lilianza kuwa Bunge la wapinzani kutokana na kuibuliwa kashfa za Epa, Buzwagi, Richmond. Hapa sasa sauti zetu ndipo ziliposikika. Bunge la 10 naliangalia kwa mtazamo miwili, hapa sasa wapinzani ndipo walipotumia kila aina ya nguvu kujitokeza mbele kupaza sauti na naamini tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa na hii sauti ndiyo itakayotupa ushindi mwaka huu. Jambo la pili, Bunge hili limeshindwa kutengeneza Katiba, Kura ya Maoni na ni Bunge lililopata joto jingi kutoka kwa wapinzani, ndani na nje ya Bunge. Swali: Unaposema nje ya Bunge unamaanisha nini? Lissu: Nikisema nje ya Bunge namaanisha, Watanzania walikuwa wanalifuatilia kwa karibu sana kupitia televisheni, sasa ndani ni joto na nje watu walikuwa na joto. Kila mtu alitengeneza ufahamu wa Bunge na ilitupa nguvu kuwa Watanzania sasa wana ufahamu. Swali: Kitu gani hasa kiliwafanya sauti zenu zisikike kipindi hiki cha karibuni ikiwa ni takribani miaka 20 tangu kuanza kwa vuguvugu la mageuzi hadi mageuzi yenyewe mwaka 1992. Lissu: Unajua tulianza kwa kusuasua sana, hatukusikika. Wakati Rais anakuja kulihutubia Bunge kwa mara ya kwanza Novemba 18, 2010, tulisusia pale na hapo ndipo tukatengeneza ufahamu mkubwa kwa Watanzania na wakaanza kutuelewa kwa nguvu na zaidi, hoja ilikuwa kumsusia Rais. Sasa, mjadala na hoja ulibadilika, ikawa upinzani kumsusia Rais, ilisikika sauti ya Rais na upinzani ulisikika na tulifanye vile kutengeneza ‘awareness’. Swali: Unadhani mlifanikiwa kwa kiasi gani? Lissu: Tulifanikiwa sana. Hapa naweza kusema sauti ya upinzani ilisikika, tulikuwa hatujui tufanye nini tusikike. Swali: Ukiacha hiyo ya Rais, mara kwa mara mmekuwa pia mkisusia vikao na kutoka nje, hii nayo mlikuwa na dhamira kama hiyo? Na kususia unadhani kuna mafanikio au kubomoa? Lissu: Tulikuwa na dhamira kama hiyo. Unajua unapodai haki kuna njia nyingi za kutengeneza mazingira usikike; kususia, kufanya maandamano na hiyo huleta changamoto kwa upande mwingine. Sasa, nikupe mfano mmoja ambao naweza kusema tumefanikiwa. Tuliposusia Bunge Maalumu la Katiba, wenzetu walidhani sasa ndiyo nafasi ya kupitisha mambo yao, lakini wapi, si hii Katiba, hadi leo hakuna kinachoendelea. Tulikuwa na nafasi yetu kama upinzani, lakini hawakutusikiliza, wakaanza kupigisha kura watu wasiokuwapo, waliokwenda Hija ili muradi yatimie, lakini mwisho wa siku hadi leo ni vurugu, nasema upinzani kwa hapa tumefanikiwa. Swali: Kwa nini msidai haki na mkawasilisha malalamiko ama hoja zenu kwa kafuata utaratibu? Lissu: Utapigwa bao. Wewe ukifuata njia hizo hakuna wa kukusikiliza. Swali: Nini mmejifunza katika Bunge la 10 hasa mwenendo mzima wa Bunge? Lissu: Unajua wapinzani hatukujengewa mazingira, tulichokiona, kama Serikali ikiwajengea mazingira wapinzani, kila waziri kivuli akawa na ofisi, tungeinyoosha Serikali. Unajua hali inavyokuwa ukimwagiwa maji ya baridi unapokuwa usingizini, sasa ndivyo ilivyo katika upinzani kwa watawala. Pamoja na kwamba mawaziri vivuli hawana ofisi, tumefanya kazi na tunachotaka sisi, si kuivuruga Serikali, tunachotaka sisi si kuishambulia tu Serikali hata tunapowabeza, ni kwamba tunawataka kuongeza kasi ya uwajibikaji na kama kasi inawashinda watuachie. Mmeona hapa, katika Bunge la 10 mawaziri wameng’oka katika kashfa mbalimbali, wameng’oka kwa tuhuma mbalimbali na nasema Bunge lenye nguvu, linazalisha Serikali yenye nguvu na Bunge lenye upinzani wenye nguvu, linazalisha Bunge lenye nguvu. Mwenendo mzima ni mzuri, lakini sasa, hii kasoro iondolewe Bunge lijalo. Mawaziri vivuli wapewe ofisi wafanye kazi zao. Wakiwa na wageni wanawapeleka kantini, kweli? Hii si sawa. Swali: Unadhani kama wapinzani, mmeichangamsha Serikali kwa kiasi gani? Lissu: Zamani ilikuwa tofauti kidogo. Tuliwapiga sana bao, kwenye kanuni na vitu vingine, wapinzani walikuwa wakisoma sana, walikuwa wakifuatilia sana mambo na kuleta bungeni kutengeneza hoja, wenzetu walikuwa hawana hulka ya kusoma kwa baadhi yao, sasa siku hizi wanatufuatilia kweli. Wanasoma hotuba zetu tena kwa umakini sana na ‘wanachallenge’ hata sisi inatupa joto kwamba tutengeneze kitu ambacho ukikiwasilisha kweli kimewagusa. Swali: Hoja zenu zinafanikiwa vipi kwa wingi wa wabunge wa CCM na idadi yenu? Lissu: Hapo sasa ndiyo shida. Unajua wenzetu wako wengi na sisi hatuzidi 100 ukiacha hao akina Cheyo (John) na Mrema (Augustine), sasa inapokuja suala la kutoa uamuzi, wanatushinda kwa kuwa wao ndiyo wengi na hoja zetu zinabakia kufa kifo cha kawaida, ila moto tunawawashia wa kutosha. Tungekuwa wengi, ingekuwa nzuri, na bunge lijalo, ninatamani liwe na uwiano sawa wa wabunge wa CCM na upinzani ili kuleta usawa kuliko hali ya sasa. Swali: Kitu gani kibaya na kitu gani kizuri ambacho hamuwezi kukisahau katika Bunge hili? Lissu: Hii naweza kusema ‘bad moment’ ya upinzani ni pale Spika alipoonyesha upendeleo kwa Serikali. Ilikuwa inatuumiza. Wakati mwingine hata kutoa hoja kunaminywa, kumekuwa na miongozo mingi hadi leo haijatolewa majibu, sasa hapo ndipo upinzani ilikuwa ikituchanganya. Sasa, Spika ajaye asimamie misingi ya kanuni na sheria, awe anajua sheria na kuondoa hali hiyo. Spika ajaye pia ajipange na moto wa upinzani ambao ninadhani mwakani utakuwa mkubwa. ‘Best moment’ ya upinzani ni pale tulipowasha moto bungeni. Aisee, upinzani unapoibana Serikali kwa hoja, akaingilia Mwanasheria Mkuu, akaingilia Mnadhimu wa Serikali, Spika, huku wapinzani wakiendelea kutoa hoja mfululizo, pale huwa tunafurahi sana, kama mimi pamoja na kwamba ninashiriki kutoa hoja na najua kabisa tumewashika, ule ugomvi pale huwa naufurahia sana. Pale sasa upinzani tunaamini tumechukua pointi. Swali: Umesema unatamani kuona Bunge lijalo liwe na uwiano sawa, mnatamani wabunge wa namna gani? Lissu: Natamani kuona Bunge la uwiano sawa wapinzani na CCM, hili ni la msingi na wabunge hasa wa upinzani natamani kuona wenye mitazamo migumu kama ya Lissu, (John) Mnyika, (Mch Peter) Msigwa, (Halima) Mdee, Mkosamali, (David) Kafulila wabunge wa namna hii watachangamsha sana Bunge. Swali: Wabunge gani wa CCM mnawakubali? Lissu: Kwa pale, wabunge wa CCM ambao tunawakubali wanaposimama ni Kangi Lugola (Mwibara) ni mwenye misimamo, James Lembeli (Kahama), Christopher Ole Sendeka (Simanjiro), Luhaga Mpina (Kisesa), Ester Bulaya (CCM). Ni wabunge wanaotaka kuona hili na hili linatokea na wanawashangaa wenzao wanatoka nje ya mstari kwa nini. Hawa tunawakubali sana. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

JK: Nikisamehe wafungwa wanaongezeka 3,000

$
0
0

Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete, ameelezea kushangazwa na ongezeko la uhalifu nchini kwamba kila anapotoa msamaha kwa wafungwa 4,000 katika sherehe za Muungano, lakini inapofika siku ya Uhuru, Desemba 9, anapewa taarifa kuna ongezeko la wafungwa 3,000. Rais Kikwete, aliyasema hayo jana wakati akifunga mafunzo ya ngazi ya juu ya uongozi wa askari magereza, yaliyofanyika katika Chuo cha Magereza Ukonga wilayani Ilala jijini Dar es Salaam. Alisema: “Kila tunapofanya sherehe mbalimbali za kitaifa, najitahidi kutafuta sababu za kuwapunguza…lakini mambo yanakuwa tofauti,” alisema Rais Kikwete huku akishangiliwa na mamia ya walioudhuria halfa hiyo. Aliongeza kuwa “magereza 126, yaliyopo hivi sasa, hayatoshelezi kukidhi mahitaji ya kukabiliana na wimbi hilo la msongamano wa wafungwa kutokana na kasi ya uhalifu kuongezeka. Alisema kutokana na hali ya misongamano ikitokea ikafanyika sensa ya kimataifa juu ya wafungwa magerezani, Tanzania inakuwa ya mwisho katika kukabiliana na ongezeko la wafungwa kwenye magereza. “Hivi sasa kuna haja ya kurekebisha na kujenga magereza mapya, ili kukabiliana na changamoto hiyo sanjari na kuboreshwa huduma za wafungwa, kwani nao ni binadamu.Hivyo kuwataka askari wa jeshi hilo kufuata taratibu na kutenda haki kwa wafungwa. “Tendeni haki kwa wafungwa hawa ili kuondoa malalamiko na maneno toka kwa ndugu zao, kwani wapo gerezani kwa ajili ya kujifunza kutokana na makosa yao,” alisema Rais Kikwete. Pia, aliliagiza jeshi hilo kuandaa mpango mkakati kama wanavyofanya polisi na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ili kujua namna za kukabilina na changamoto zinazowakabili. “Mpango wenu ukikamilika msipite njia ndefu… nileteeni mimi moja kwa moja nijiue namna ya kuufanyia kazi, kabla ya kuondoka madarakani,” alisema Rais Kikwete. Kamishna Jenerali wa Magereza, John Minja, alisema jumla ya askari 104 walihitimu na kupewa vyeti, kati yao 10 wanatoka katika vyuo vya mafunzo Zanzibar. Alisema mafunzo yana lengo la kuwaanda wanafunzi hao kuwa askari bora katika jeshi hili, na kozi ilitolewa kwa miezi minne , huku wakifundishwa masomo ya utawala wa magereza, haki za binadamu, afya ya jamii na utawala wa fedha. “Mbali na kusoma darasani pia, walifanya mitihani yao kwa vitendo,” alisema Kamishna Minja. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat


Urais 2015: Membe Adai Pinda Anamnyima Usingizi

$
0
0

WAZIRI wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ambaye pia anaomba CCM impitishe kuwa mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu baadaye mwaka huu, Bernard Membe amekiri kwamba katika kinyang’anyiro cha urais ndani CCM, mtu anayemnyima usingizi ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda. Akizungumza na wanachama waliojitokeza kumdhamini jana, Membe alisema Pinda asingechukua fomu ya urais ndani ya CCM, angefurahia ushindi tu na tayari angekuwa ameshona suti na kushangilia ushindi. Alisema kuwa Waziri Mkuu Pinda ni mchapakazi, asiye mbinafsi, mwadilifu, mvumilivu sana mwenye hekima na busara ya hali juu, mwanasheria aliyebobea na ndiye mwalimu aliyemfundisha kazi. “Wengine wote hawanitishi nitawagonga lakini nikifika kwa Pinda itabidi nipumue kwanza…kwa hiyo mimi na Pinda ni pacha nikishindwa mimi nitamuunga mkono lakini akishindwa naamini ataniunga mkono, ndio maana hata wakati nakuja huku nimewasiliana naye akanieleza nenda na amenisaidia nimepata wadhamini wa kutosha,” alisema. Membe amesema kuwa Mungu akimjaalia kuteuliwa na CCM kushinda urais atahakikisha baadhi ya miradi inayotumia fedha za ndani ambayo inasuasua ikiwemo ujenzi wa barabara ya Sumbawanga hadi Mpanda unakamilika, lakini pia bonde la Ziwa Rukwa linatumika kuzalisha chakula ambacho kitalisha nchi nzima kwa kuwa ardhi yake ina rutuba na inafaa kwa kilimo. Pia, Membe aliwaasa baadhi ya wanaCCM kuacha kuwashangilia kila mgombea anayepita kuomba udhamini kwa kuwa si wote wana sifa kwani wenye sifa stahiki ni yeye na Waziri Mkuu Pinda. Awali, Katibu Mwenezi wa Mkoa huo, Clement Bakali alisema kuwa mgombea huyo amepata wadhamini 855 kutoka wilaya zote za mkoa wa Rukwa. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Magaidi Yaitikisa Tena Morogoro

$
0
0

POLISI mkoani Morogoro kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama imekamata washukiwa wa ugaidi waliokuwa na mifuko mikubwa iliyokuwa na majambia na bunduki kadhaa aina ya Shot gun.   Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Mussa Marambo, alisema hayo jana mjini hapa na kufafanua kwamba ni washukiwa sita kati ya 50 waliotiwa mbaroni, huku msako ukiendelea kuwatafuta wengine.   Kwa mujibu wa Kamanda Marambo, Jumatano iliyopita Polisi iliarifiwa na raia wema kuhusu uwepo wa watu hao katika Msitu wa Njeula katika kijiji cha Njeula tarafa ya Turiani, wilayani Mvomero.   Kukamatwa Baada ya taarifa hiyo, Kamanda Marambo alisema Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama, walifika eneo la msitu huo kufuatilia nyendo zao ili kuwakamata.   Hata hivyo, katika harakati za kuwakamata Kamanda Marambo alisema washukiwa hao walifanikiwa kutoroka, isipokuwa mmoja ambaye alitiwa mbaroni.   Katika purukushani hiyo msituni, Kamanda Marambo alisema mshukiwa huyo aliyekamatwa, alijaribu kumjeruhi askari kwa kumkata na jambia mkononi, lakini umakini wa askari Polisi ulisaidia kumuepusha mwenzao asijeruhiwe na kukamata mshukiwa.   Msako wa watu hao uliendelea ambapo Kamanda Marambo alisema baada ya muda, washukiwa wengine watano kati ya 49 waliokuwa wametoroka, walitiwa mbaroni huku wengine 44 wakitokomea porini.   Walikotokea  Uchunguzi wa awali wa Polisi, umebaini kuwa washukiwa hao wakiwa na mifuko hiyo mikubwa iliyohifadhi majambia na bunduki, walitokea wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, kupitia Tanga huku wakitumia mabasi ya kuunganisha.   Kutoka Bagamoyo, Kamanda Marambo alisema washukiwa hao walizunguka kwa kwenda mpaka Segera mkoani Tanga, wakaingia Handeni ndipo wakatokea katika kijiji cha Njeula tarafa ya Turiani wilayani Mvomero.   Msako shirikishi  Kwa mujibu wa Kamanda Marambo, msako mkali unaendeshwa katika msitu huo na mahali pengine ili kufanikisha kutiwa mbaroni kwa washukiwa waliobaki.   “Ninachoweza kusema kwa kushirikiana na wenzetu wa Tanga, bado tunaendelea na msako kwenye msitu huo uliopo mpakani lakini siwezi kujata majina yao kwa sasa wala kueleza wanatoka wapi au nia yao ni nini,” alisema.   Kamanda Marambo pia alikataa kutaja idadi ya majambia wala bunduki hadi watakapokamilisha uchunguzi na upelelezi wa suala hilo.   Hivyo aliwataka wananchi wenye mapenzi mema na Taifa lao, kuendelea kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama ili kufichua watu wanaowatilia shaka wanapowakuta misituni na mitaani, ili hatua za haraka zichukuliwe.   Hii ni mara ya tatu kwa wanaoshukiwa na vitendo vya kigaidi kukamatwa mkoani Morogoro, ambapo hivi karibuni washukiwa wengine 25 walikamatwa kwa nyakati tofauti katika eneo la Kidatu wilayani Kilombero na wameshafikishwa mahakamani FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

TID: Ni Kweli Navuta Bangi

$
0
0

Kwa mara ya kwanza, ‘mnyama’ katika anga la muziki wa Bongo Fleva, Khaleed Mohamed ‘Top In Dar’ (TID) amekiri kutumia mihadarati aina ya bangi huku akijiapiza kuwa hajawahi kutumia madawa mengine ya kulevya ‘unga’ ikiwemo cocaine kama ambavyo amekuwa akinyoshewa vidole na baadhi ya watu. Akizungumza na Gazeti  la  Ijumaa katika mahojiano maalum wikiendi iliyopita, TID ambaye ni mmiliki wa Top Band alifunguka kuwa miongoni mwa mambo yanayomkosesha raha na amani ya moyo, ni pamoja na kuhukumiwa kujihusisha na matumizi ya unga na wengine kwenda mbele kwa kusema hata kushuka kwake kisanii kumechangiwa na ishu hiyo. Staa huyo wa Ngoma ya Kiuno alisema kuwa, wakati mwingine watu wanamsakama hadi mama yake mzazi wakimtaka amkanye mwanaye kujiepusha na maisha ya ‘kubwia unga’ jambo ambalo linampa wakati mgumu na kujiona kuonewa katika jamii. Kuhusu kushuka kimuziki, TID alisema miongoni mwa sababu zilizosababisha kuporomoka katika anga la muziki ni kile alichokiita ‘hujuma’ kutoka kwa baadhi ya wadau wakubwa wa muziki (majina yapo), kwa kushindwa kumpa fursa za kimuziki zikiwemo promosheni na mialiko ya shoo kwa kuwa wana vinyongo na fitina dhidi yake. “Kaka, naonewa kabisa nikihusishwa natumia madawa ya kulevya, wanamsumbua mama eti akae na mimi anionye. “Jamani situmii madawa ya kulevya kama cocaine, ila kwa upande wa bangi ni sawa nakubali kuwa navuta. “Lakini pia, kuvuta kwangu bangi siyo sababu ya mimi kushuka kisanii, zipo sababu zingine kabisa kama kuhujumiwa na wadau wakubwa wa soko la muziki kutokana na mabifu yanayotokana na sababu binafsi. “Hivi kweli mtu anayetumia madawa ya kulevya kama cocaine, anaweza kumudu maisha kama kununua nyumba? Kununua magari? Hata kuendelea kuimba kweli? Siyo sawa jamani,” alisema TID. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Wagombea Urais Wafika 42 CCM

$
0
0

MWANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Banda Sonoko, jana amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa na chama hicho ili kugombea urais kwenye Uchaguzi Mkuu ujao akiwa ni mgombea wa 42. Baada ya kuchukua fomu hiyo jana, Sonoko alisema kama chama hicho kitampitisha kuwa mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu ujao na kushinda, moja ya vipaumbele vyake ni pamoja na kuzingatia misingi imara ya ilani ya 2005 pamoja na kuondoa umaskini kwa Watanzania. Sonoko amewahi kushika nyadhifa mbalimbali ikiwemo ya Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Temeke ambapo katika kampeni zake za kusaka urais atatumia kauli mbiu inayosema “Kutokomeza Umaskini”. Alisema akiingia Ikulu, atawatimizia Watanzania mahitaji mbalimbali ambayo wameyakosa muda mrefu ambapo yeye ana sifa zote za kuwa rais ndio maana ameamua kuchukua fomu. Aliongeza kuwa atahakikisha nchi inaendeshwa kwa kodi za wananchi si misaada kutoka nchi wahisani ambapo wanawake watawezeshwa katika mambo mbalimbali na kupewa nyadhifa kwenye vyombo vya maamuzi pamoja na vijana. Sonoko alisema Serikali ambayo ataiongoza itasimamia haki, kupinga vitendo vya utoaji na upokeaji rushwa hasa Mahakamani ambapo kesi zitakuwa zikiendeshwa kwa muda maalumu, kurudisha viwanda, kuinua kilimo na kuboresha miundombinu. “Nitahakikisha kila Wilaya inakuwa na sehemu yake ya kuegesha magari, kuongeza ajira na kuwasaidia vijana,” alisema na kuongeza kuwa, hadi Julai mosi, mwaka huu, atakuwa amekamilisha taratibu za kupata wadhamini 450 katika mikoa 15. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Mpinzani wa Rais Museveni kuitikisa Uganda akitokea Ulaya

$
0
0

Taharuki imetanda mjini Kampala Uganda baada ya habari kuenea kuwa mpinzani mkuu wa rais Yoweri Museveni ,aliyekuwa waziri mkuu Amama Mbabazi anarejea leo.   Inadaiwa kuwa  polisi wametumwa katika barabara ya kutoka Kampala hadi kwenye uwanja wa ndege wa Entebbe.   Bwana Mbabazi anasemekana kuwa anarejea kutoka kwa ziara ya kimataifa iliyompeleka Uingereza na Marekani huku wafuasi wake wamepanga kumkaribisha kwa shangwe na vigelegele.Pamoja na msafara wa magari yaliyojaa wafuasi wake kumkaribisha.   Amama Mbabazi alitangaza majuma mawili nia ya kushindana na rais Museveni kuwania uwenyekiti wa chama cha National Resistance Movement na hatimaye kuwania kiti cha urais. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Mtoto wa Rais Kikwete ashinda medali Marekani

$
0
0

Mtoto wa Rais Jakaya Kikwete anayesoma shule ya kimataifa ya Feza, Khalfan Jakaya Kikwete (17) ameiwakilisha vema Tanzania katika shindano la kusaka wanafunzi wenye akili nyingi ‘Genius Olympiad’ lililofanyika Oswego, Marekani mwaka huu.  Shindano hilo huandaliwa na Idara ya Sayansi na Elimu ya Chuo Kikuu cha New York likishirikisha shule za kimataifa duniani likihusisha kazi za masuala ya sayansi, sanaa, biashara na mazingira.  Kwa mujibu wa mtandao wa www.geniusolympiad.org, mwaka huu nchi 69 zilishiriki kwa kupeleka kazi 1,171. Kazi 401 zilikidhi vigezo na kupokewa. Shule za kimataifa za Feza ziliwasilisha kazi nne na kushinda medali moja ya dhahabu na tatu za shaba.  Kazi iliyoshinda medali ya dhahabu iliitwa ‘Vcardin’ iliyoandaliwa na kuwasilishwa na Khalfan na Seif Yahya Mhata ambao wote ni wanafunzi wa shule za Feza.  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, Khalfan alisema kazi yao imelenga kurahisisha mawasiliano ya kimataifa kwa kuwa na njia ya uhakika ya kuwasiliana. “Mradi huu unahusu kubadilishana kadi za mawasiliano kwa njia ya mtandao. Ni muhimu sana kwa mawasiliano hasa ya wafanya biashara, lakini inahitaji uwe na simu ya kisasa yenye intaneti au kifaa kingine chenye intaneti,” alisema Khalfan aliyekuwa amefuatana na Mhata. Kazi nyingine kutoka Feza zilizoshinda medali za shaba ni ‘The Fault of Humanity’ iliyoandaliwa na Prince Mwemezi ambaye alipiga picha ya moto ukiunguza miti eneo la Tanganyika Packers, Kawe jijini Dar es Salaam na kuonyesha athari za mazingira zitokanazo na uchomaji misitu. Medali nyingine ya shaba imeletwa katika shule ya Feza na wanafunzi wawili Goodluck Komba na Sajjad El-Amin ambao walianza kazi inayoonyesha namna mkaa unavyoweza kupatikana kupitia karatasi na takataka badala ya kukata miti.  Veronica Ndomba, mhitimu wa kidato cha sita mwaka huu katika shule ya Feza Girls, aliandaa kazi ya kuzuia uchafuzi wa mazingira ya bahari kwa kuelimisha watu kuhusu kutotupa taka, mafuta na uvuvi haramu baharini na kushinda medali ya tatu ya shaba. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Majibu ya Zari kwa wanaomshutumu kutoheshimu Mwezi wa Ramadhan yanashtua

$
0
0

Zari the Bosslady amejikuta kwenye kitimoto kutokana na mashabiki kumshambulia mtandaoni kwa mavazi yake katika mwezi mtukufu wa Ramadhan. Mama huyo mtarajiwa wa mtoto wa Diamond amelazimika kutumia Kiswahili kuwajibu wale wanaomshambulia kwa mavazi yake katika kipindi hiki ambacho waislamu duniani kote wapo kwenye mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan. “Mnikome, maisha yangu yanakuhusu nini wewe, na yako hayanihusu mimi kabisa ata kidogo,” ameandika Zari kwenye Instagram.   “Oh sijui high heels, mara nguo imembana, sijui anapikia heels,pili pili hujakula wewe inaakuwashia nini? Mvae madera zenu mfunge mkanda mpite kimya kimya. Kwanini unastress???? HAYA NI MAISHA YANGU,” ameongeza.   “Na sasa your all Gods’ judges now…. how many people do we know that wear hijab but have very dirty ugly hearts? Huh? How many of you act so straight for these 30 days but the last 11 months you’re the worst monsters this world has ever seen. Now u wana come here and judge my faith by the dress?” “Allah bless all of you….atleast I ain’t acting snitchy, am being ME. And oh, if you happen not to like what you see in ur news feed (my page) U always have 3 options, Block yourself, unfollow ama fast forward coz if your still following na you exercise your fingers kuwakya matusi page yangu, babe your just an obsessed fan if not a confused admirer dah majirani. Habari nakazi mnayo……like I always say, no bad vibes from me. So stay blessed.” FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat


Dira ya Dunia Tv kuzindua sura mpya leo

$
0
0

Idhaa ya Kiswahili ya BBC Swahili itazindua sura mpya ya “Dira ya Dunia” leo! Kipindi hicho kinachopeperusha taarifa ya habari kwa zaidi ya watazamaji milioni 6.9 itakuwa na sura mpya inayojumuisha maandishi mapya yaliyotiwa nakshi,vipindi vipya na ripoti za kina zinazojumuisha habari, michezo na burudani. Tangu ilipozinduliwa mwaka wa 2012 Dira ya Dunia TV, inatazamwa kila siku na mashabiki kanda ya Afrika Mashariki na Kati matika mataifa ya Tanzania, Kenya, Burundi na katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo. Aidha “Dira ya Dunia” ina mashabiki si haba katika mitandao ya kijamii. Mtangazaji nyota wa idhaa hii ya Kiswahili, Salim Kikeke, alitunukiwa mataji ya ”Tuzo Za Watu” na Mtangazaji bora wa runinga wa mwaka, kwa mwaka wa pili mtawalio. Mshindi wa tuzo hizo anachaguliwa na umma. Kikeke anasaidiana na watangazaji wenza, Kassim Kayira, Zuhura Yunus na Peter Musembi. Dira Ya Dunia yenye sura mpya itaendelea kuwaletea wageni wenye uzoefu wa maswala tofauti. Wageni waliohojiwa tayari katika Dira ya dunia ni pamoja na rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, rais Pierre Nkurunziza wa Burundi na rais Yoweri Museveni wa Uganda mbali na wasanii waliobobea kama vile Diamond Platnumz kutoka Tanzania, Eddy Kenzo kutoka Uganda na Juliani wa Kenya. “Siamimi kwa hakika kuwa imekuwa takriban miaka mitatu tayari . ”Imekuwa safari ya kuvutia sana.” ”Mapokezi yetu katika kanda zima ya Afrika Mashariki na kati ni ya kufana na kuridhisha.” ”Tunapania kuendelea kuwapasha habari wasikilizaji wetu kuwa elimisha na pia kuwa burudisha kwa miaka mingi.” ”Hii sura tunayoizindua ni thibitisho tosha kuwa ari yetu ni hiyo” anasema mtangazaji kinara Salim Kikeke. Kwa upande wake Mhariri na Mtayarishi mkuu wa Dira ya Dunia Tv bi Mariam Omar anasema kuwa ”inafurahisha mno kwa mtazamaji kuwa tunaimarisha kipindi chetu maarufu ”Dira ya Dunia TV .” ”Tutaendelea kuwapa watazamaji wetu habari za utendeti zaidi na kwa njia za kuvutia watazamaji wetu ambao bila shaka watakuwa na uwezo zaidi wa kuwasiliana nasi na kuchangia habari tutakazo peperusha.” FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Je,unaweza kuishi ukiwa uchi?

$
0
0

Watu wengi wasingejihisi vyema kuvua nguo zao zote na kusalia uchi wa mnyama katika maeneo ya uma,lakini kwa wengine ni maisha yao. Mwandishi kutoka nchini Marekani Mark Haskel Smith alikabiliana na changamoto zote na kuweza kuishi bila nguo.Iwapo upo katika uwanja wa ndege ,huwezi kufanya masihara kuhusu bomu. Na iwapo uko na watu walio uchi huwezi kufanya masihara kuhusu matiti. Na mungu wangu,usisisimkwe,utaamrishwa uondoke asema Haskell Smith. Haya ni mambo mawili aliyogundua alipotembelea maeneo ya kupumzika ya watu walio uchi duniani. Ziara yake ya kwanza ilikuwa katika mkahawa wa Desert Sun Resort huko Palm Springs Carlifonia. ‘Nilishtuka’.’Nilikuwa na wasiwasi katika chumba changu cha hoteli,nikijipaka mafuta baada ya mafuta hadi nilipotoka nje,nilikuwa niking’ara sana”,. ”Kuna watu chungu nzima katika kidimbwi cha maji wwaliokuwa ndani ya kidimbwi kimoja cha maji walioniangalia na kujifunika nyuso zao. Nilijihisi vibaya sana,nilifikiri watu hawa wamenipita na zaidi ya miaka 20 lakini nilipojiangalia chini ”ooh mungu wangu”. Baada ya kuzuru eneo hilo alizuru maeneo mengine ya watu walio uchi barani Ulaya. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Gatlin aweka mda bora mita 200

$
0
0

Mwanariadha wa mbio fupi Justin Gatlin ameweka mda bora zaidi katika mbio za mita 200 na kuwa wa tano duniani aliposhinda mbio hizo nchini Marekani. Raia huyo wa Marekani mwenye umri wa miaka 33 ambaye amehudumia marufuku mbili za utumiaji wa dawa za kusisimua misuli aliweka rekodi ya mda wa sekunde 19.57 mjini Oregon. Rekodi hiyo imeifuta ile ya sekunde 19.68 aliyoiweka mnamo mwezi May wakati huo ikiwa rekodi bora duniani. ”Nilitaka kutoka ili niweke historia,na hivyo ndivyo nilivyofanya”,alisema Gatlin. Gatlin ndiye mwanariadha wa mbio fupi aliyetawala mwaka 2015 baada ya kuweka rekodi bora mwaka huu ya sekunde 9.74 katika mbio za mita 100. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

ARM’s New Chip Design Extends Battery Life of IoT Devices

$
0
0

An overhaul of the company’s chip design results in significantly longer battery life in IoT devices such as health monitors, smart home devices and sensors. ARM is trying to resolve the thorny problem of battery life in Internet of Things devices with a new chip design that will significantly reduce the power consumed by processors, sensors and wireless chips. The company has overhauled the way it designs low-power Cortex-M chips that go into IoT devices such as health monitors, smart home devices and sensors. The restructured design could almost double battery life, ARM executives said at Computex in Taipei on Monday. For example, the battery life of a connected hearing aid could more than double with chips based on the new design, said Jeff Chu, director of marketing at ARM. Chu provided another example of a smart lightbulb lasting a lot longer on a battery charge with new chips based on the design. The smart bulb could have solar cells to refresh the battery, and the chip’s lower power consumption could help the battery last for years. The restructured Cortex-M also boasts support for a new Bluetooth 4.2 radio called Cordio, and has a new memory subsystem that will enable faster exchange of data between components. Additionally, a wide range of sensors can be applied to the chips. ARM showed chips based on the new design at a news conference at Computex. A developer board with the Cordio-based Bluetooth chip was able to measure ambient temperature and transmit the readings to a smartphone. The company intends to add more wireless connectivity options to its IoT chip designs too, Patel said. It hopes to add support for the 802.15.4 standard, which is the basis for Zigbee, a low-power wireless data transfer protocol that competes with Bluetooth. With the redesign, ARM is also trying to speed up the development of chips for IoT devices, which could number more than 50 billion by 2020, said Dipesh Patel, executive vice president of technical operations at ARM. ARM designed the new development platform to work with its mbed OS for the Internet of Things. A wine rack on display at the news conference used the Raspberry Pi and mbed OS to check the inventory and temperature of a wine rack, with the information transmitted to apps on mobile devices via the Amazon cloud service. Why It Matters With the Internet of Things set to number in the billions of connected device within the next decade, battery life will be at a premium. ARM’s release foretells good news in the race to extend device power longevity.  FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Kinana aitolea uvivu Serikali ya CCM

$
0
0

Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana ameikosoa Serikali ya chama chake kwamba imekuwa siyo sikivu kwa matatizo ya wananchi na kuwa wabunge wa chama hicho wanapitisha sheria ambazo zinakuwa mzigo kwa wananchi. Akihutubia katika mkutano wa kuhitimisha ziara yake, jijini Mwanza jana, Kinana alisema atafanya kikao cha kwanza na wabunge wa CCM baada ya uchaguzi ili kuwaeleza majukumu yao ya msingi ikiwamo kuiwajibisha Serikali. Alisema wabunge wa CCM wamekuwa wakiunga mkono kila jambo linaloletwa bungeni bila kutathmini matokeo ya sheria hizo kwa wananchi wanaowawakilisha. Alisema lazima ifike wakati wabunge wa CCM wabadilike na kuwatumikia wananchi wao. “Nitakutana na wabunge wa CCM na kuwaambia kwamba sheria walizozipitisha haziwasaidii wananchi… lazima chama kiwe na nguvu ya kuielekeza au kuiwajibisha Serikali yake,” alisema Kinana huku akishangiliwa na wananchi waliohudhuria mkutano huo. Katibu Mkuu huyo alisema kuna haja ya kubadilisha mfumo wa utendaji kazi wa chama na mojawapo ni kuchagua mtu mwingine wa kuongoza wabunge wa CCM bungeni badala ya Waziri Mkuu kama ilivyo sasa. Alisema Waziri Mkuu ataachwa atekeleze jukumu lake la kuiongoza Serikali bungeni, lakini kuwe pia na kiongozi wa wabunge wa CCM bungeni. Alisema mfumo huo utakipa chama nguvu zaidi ya kuisimamia Serikali yake. “Wamekaa wabunge tena na kupitisha sheria ya kila gari kuwa na kizimamoto, nani alisema gari langu lina mpango wa kuungua?” alihoji kiongozi huku na kusema sheria nyingine zinatakiwa kufutwa kwa sababu hazimsaidii mwananchi. Aliishangaa Serikali ya CCM kwa kushindwa kufuta baadhi ya sheria ambazo zimebainika kuleta usumbufu kwa wananchi na kusisitiza kuwa lazima ifike wakati Serikali ifanye tathmini ya sheria zake na kuzifuta ambazo hazifai kwa sasa. “Nimekuwa waziri na kiongozi serikalini kwa muda mrefu, lakini sijawahi kuona Serikali ikifuta sheria. Wamekuwa wakiongeza sheria mpya kila siku. Hivi karibuni Serikali imepeleka miswada mingine 11 na yote imepitishwa. Kwa namna hiyo tunambebesha mwananchi mzigo mkubwa,” alisema. Kinana aliitaka Serikali kuwashirikisha wananchi wakati wa kutunga sheria ili kuondoa changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza mara kwa mara. Kuhusu ahadi za Rais Kinana alisema Serikali imefanya mambo mengi katika kuliletea Taifa maendeleo kwa kutekeleza kikamilifu Ilani ya CCM ya mwaka 2010 na ahadi nyingine zilizotolewa na Rais Jakaya Kikwete wakati wa kampeni za urais. Alisema wakati Serikali ikiingia madarakani mwaka 2005, kulikuwa na wanafunzi wa elimu ya juu 48,000 tu, lakini sasa wanafikia 200,000. Aliongeza kuwa zaidi ya vijiji 1,000 vimeunganishwa na umeme. “Katika kipindi cha miezi 26 ambayo tulikuwa tunatekeleza maazimio ya mkutano mkuu wa mwaka 2012, nimejifunza mambo mengi. Nimeyajua matatizo ya wananchi kwa karibu zaidi, lazima Serikali iwe sikivu,” alisema Kinana. Akimkaribisha Kinana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye aliwataka Watanzania wasimame imara kukataa senti tanotano kutoka kwa wanaotaka kununua uongozi ambao baadaye wanataka kurudisha fedha zao. “Ndiyo maana tunakumbana na ‘skendo’ kibao, kesho Escrow, keshokutwa Richmond, vyote hivi dawa yake moja, lazima tuzuie wanaotaka kununua uongozi… na kama hiki ndicho wanachokitaka, safari hii tutazuia wanaotaka kununua uongozi. “Hatuwezi kuzunguka nchi nzima kusafisha chama halafu, wachache wanakaa chini wanasema nitanunua hawa, halafu sita nitakuachia… watashika adabu mwaka huu na hii itakuwa fundisho. “Niko tayari kuliongoza jeshi la vijana kukataa biashara ya kununua uongozi na matumizi mabaya ya fedha kwenye uchaguzi… haya ndiyo yanayoharibu maadili ya nchi hii kwamba mtu anaamua yake na mwaka huu Mungu atawalaani,” alisema Nape. Nape aliwatahadharisha wananchi kuepuka siasa za ushabiki kwani wakati wao (wananchi) wakiathirika, watu wachache ndiyo wanaonufaika. Alisema CCM imejipanga kuja kivingine katika jitihada za kuwatumikia wananchi. “Chama cha Mapinduzi hakiuzi uongozi. Natoa wito kwa wale wote wanaofikiri kuwa wanaweza kufanya hivyo watambue mapema kwamba haiwezekani,” alisema. Akimpongeza Kinana kwa juhudi zake za kukiimarisha chama kwa kutoka ofisini na kwenda kwa wananchi, Nape alisema ziara za katibu mkuu huyo zimetumia miezi 26 na siku 18 katika mikoa 31 nchini. alisema katika ziara hizo, ametembea umbali wa kilomita 193,574 huku akizindua miradi 2,671 na kuingiza wanachama wapya 208,432 na kati yao, 38,934 walitoka Chadema. Katika mkutano huo, Nape alimtambulisha mwimbaji mpya ambaye atarithi mikoba ya marehemu John Komba kuongoza bendi ya TOT katika uhamasishaji wa chama. Alimtaja mrithi huyo kuwa ni Twalib Neka na kusema kuwa ameshakamilisha albamu yake ya kwanza akiwa na bendi hiyo. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Viewing all 553 articles
Browse latest View live