Quantcast
Channel: iphone – AutomobileHeat
Viewing all 553 articles
Browse latest View live

Afande Sele aeleza atakavyokuwa tofauti na wasanii wengine walioingia bungeni

$
0
0

Afande Sele amesema akiingia bungeni hawezi kuwasahau wasanii wenzake kama walivyosahauliwa na wasanii wabunge waliotangulia kuingia mjengoni. Rapper huyo  atawania kiti cha ubunge wa jimbo la Morogoro Mjini kwa tiketi cha ya chama cha ACT na amesemakuwa akiingia bungeni wasanii watarajie mambo makubwa kutoka kwake.   “Lengo langu kubwa kwa wasanii ni kupigania haki za wasanii,” Amesema  Afande Sele   “Nimegundua tukizungumzia haki za wasanii kwenye muziki kwa kuimba tu, hakuna kitachofanyika. Viongozi hawana shinikizo la kutekeleza, wanazungumzia tu kidogo halafu wanaacha.    “Lakini nimeona ukiingia bungeni wasanii tutashiriki moja kwa moja kwenye utungaji sheria za nchi.    “Suala la haki za wasanii nitakuwa niko nalo karibu sana na nitalipigania kwa namna yoyote kwa sababu nipo kwenye chombo cha maamuzi na nina rungu mkononi,” ameongeza msanii huyo.   “Lakini leo hii hata nikiwa nazungumza sina silaha yoyote, lakini tukiingia bungeni tunaweza kupaza sauti na zikasikika kwa sababu tupo kwenye chombo cha sheria na kina mamlaka na uwezo.    “Unajua kila anayeingia bungeni unakuta baadaye anabadilika, mimi nina upeo mkubwa tofauti na wabunge wanaomaliza muda wao. Inaonyesha waliingia kwenye siasa kwaajili ya kutafuta maslahi. Kwahiyo wasanii watarajie kuona sheria za haki miliki zikipatikana au zile zilizopo zikifanyiwa marekebisho,” amesisitiza.   “Kwa sasa hivi bungeni hakuna mtu mwenye uchungu na sanaa, wasanii ambao walibahatika kuwa wabunge wameingia bungeni nao wamegeuka mafisadi vilevile.   “Wamekuwa wawekezaji wa biashara, wamedharau shida za wasanii. KwaHiyo mimi nafikiri bungeni kulikuwa hakuna wasanii ambao wanatuwakilisha, wasanii tunaotaka kuingia bungeni sasa hivi tuna wito. Kwahiyo watu wategemee kuona mabadiliko makubwa sana kwenye sanaa.”   Katika hatua nyingine, Afande amesema kwa sasa hatoweza kutoa wimbo wowote mpaka uchaguzi utakapopita.   “Ningependa sana mashabiki wa muziki wangu wasubiri uchaguzi upite ndio wasikie kazi mpya kwa sababu tayari akili na mawazo na malengo yangu yapo kwenye uchaguzi. Mimi nimeona nisiwa-disturb kwa kitu chochote mpaka uchaguzi upite.    “Kwa sababu hili ni jambo muhimu sana linatokea kwenye taifa na ni maisha yao. Kwahiyo watu wajitokeze kujiandikisha pamoja na kupiga kura ili kuwachagua viongozi wanaowataka.” FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat


.Ukawa: NEC inatuvurugia mipango majimboni

$
0
0

Dar es salaam. Mwenyekiti mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), ameishukia Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kushindwa kutangaza mgawanyo wa majimbo, akisema kuchelewa huko kunavuruga mipango yao. Ukawa, inayoundwa na vyama vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, imekubaliana kusimamisha mgombea mmoja kuanzia ngazi ya urais hadi diwani na viongozi wa vyama hivyo wameshakutana mara kadhaa kuzungumzia kugawana majimbo kulingana na nguvu ya chama kwenye eneo husika. Hata hivyo, vimeshindwa kumalizia kazi hiyo kutokana na kutokamilika kwa mgawanyo wa majimbo kama NEC ilivyoahidi Mei 12 kuwa majimbo mapya kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 yangetangazwa Juni 30. Akizungumza jana, Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema aliitupia lawama NEC akisema wakati huu ilitakiwa kuwa imeshamaliza suala la majimbo na kushughulikia mambo mengine. “Tunataka kutengeneza ratiba ya mpango kazi, lakini tunashindwa. Tunataka tujue majimbo mapya ili twende huko, lakini sasa tunashindwa na muda unakwenda,” alisema Mbowe. Akizungumzia ukimya wa kutangaza majimbo hayo licha ya kusema ingefanya hivyo Juni mwishoni, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva alisema hadi sasa Tume hiyo haijakamilisha ugawaji wa majimbo lakini bado wanaendelea na mchakato huo. Alisema Tume yake imeamua kugawa majimbo hayo kwa kuzingatia vigezo mbalimbali, ikiwamo idadi ya watu, upatikanaji  wa mawasiliano, hali ya kijiografia na kanuni za uchaguzi wa Rais na wabunge za mwaka 2010. Jaji Lubuva pia alisema Tume itayagawa majimbo hayo kwa kuzingatia uwepo wa miundombinu bora, hali ya kiuchumi kwa kuweka uwiano kati ya eneo moja na jingine, mawasiliano ya simu na vyombo vya habari kwa ajili ya kupata mwakilishi atakayeharakisha maendeleo katika eneo husika. Wakati ikisuasua kutangaza majimbo mapya ya uchaguzi, NEC pia inakabiliwa na kibarua kingine cha kumalizia uandikishaji wapigakura kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura. Kazi hiyo imekumbwa na matatizo kadhaa na inatakiwa ikamilishwe katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, lakini imeahirishwa kutokana na kuchelewa kwa mashine zinazotumika za teknolojia ya mfumo wa kuchukua alama na taswira za mpigakura (Biometric Voters Registration). Jaji Lubuva alisema kuwa kuna baadhi ya majimbo ambayo ni makubwa, jambo ambalo alisema linatokana na ongezeko la watu nchini. Ugawaji wa majimbo unatakiwa kufanyika mara kwa mara au angalau mara moja baada ya miaka 10. “Ugawaji wa majimbo ulifanyika kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 na kwa kuwa sasa tunaelekea uchaguzi mwingine, lazima tufanye hivyo,” alisema  Jaji Lubuva. Kauli ya Mbowe Akizungumzia kusuasua huko kwa ugawaji majimbo, Mbowe alisema NEC inataka ifanye mambo mengi kwa wakati mmoja. “Tume imezidiwa na majukumu; inataka kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja, huku muda ukiwa haupo. Kila siku wanaahirisha hili mara lile na mengine hawayatolei taarifa,” alisema Mbowe. Alisema tangu Tume hiyo ilipotangaza kugawa majimbo ya uchaguzi nchi nzima, bado mpaka leo haijafanikisha shughuli hiyo, jambo ambalo linasababisha kuchelewa kwa umoja huo kugawana majimbo. “Uchaguzi ni vita,” alisema Mbowe. “Sasa sijui wanasubiri nini? Mpaka leo hawataki kutangaza hayo majimbo waliyosema wanayagawa, sisi tunasubiri wakimaliza tu tunaanza mchakato wa kugawana ila kwa hali ilivyo sasa, hatuwezi kufanya lolote.” FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Nyumba ya mwandishi wa Nyerere yauzwa kinyemela

$
0
0

Dar es Salaam. Nyumba ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa Mwalimu Julius Nyerere, Paul Sozigwa imeuzwa katika mazingira ya kutatanisha na mke wake Monica Kuga baada ya mwanahabari huyo kupata maradhi ya kupoteza kumbukumbu. Kuga aliiuza  nyumba hiyo kwa Mahamood Duale kwa Sh600 milioni mwaka 2010, huku watoto wake wanne wa Sozigwa wakipinga uuzwaji huo wakidai kuwa baba yao aliwakabidhi nyumba hiyo mwaka 1998. Mtoto wa mwisho wa Sozigwa ambaye pia ametajwa kama msimamizi wa mirathi, Moses alisema wana vielelezo vya wosia aliowaachia baba yao akiwa Finland kabla ya tatizo lake la kupoteza kumbukumbu halijawa kubwa. “Tulirekodi kila kitu na ushahidi wa maandishi upo, baba alisema nyumba ile ni ya watoto na siyo yake wala ya mke wake. Lakini pia tulirekodi sauti yake, tunashangaa kwanini mama ameiuza,” alisema Moses. Kwa maelezo ya wanafamilia hao, Kuga aliachana na Sozigwa mwaka 1974 na kufungua kesi ya kudai talaka mahakamani jambo ambalo baba yao alilipinga. “Alitaka kuachana na baba tena sisi tukiwa wadogo ili wagawane mali, lakini baba hakukubali, tunashangaa iweje leo arudiane naye halafu auze nyumba?” alihoji Moses. Moses alieleza kuwa mama yao alimchukua Sozigwa na kuishi naye kama kisingizio cha kujihalalishia  uuzwaji wa nyumba hiyo iliyopo maeneo ya Kurasini, karibu na shule ya Sekondari ya Jitegemee. “Mama alimkana baba na wameachana kwa miaka zaidi ya 34 na aliidai talaka hadi mahakamani kwa nguvu, halafu baba alipoanza kuumwa anadai anataka kumlea kumbe ni ujanja wake  tu, alitaka kuuza eneo la familia,” alidai mtoto huyo. Kwa mujibu wa wanafamilia hao, Kuga alighushi hati ya nyumba hiyo na kuiuza kwa Duale lakini baadaye aliwataka wampe hati halisi ili amkabidhi Duale. Lakini baada ya kuona kuwa hawezi kuipata, kwa kushirikiana na Duale walianza kumsumbua Moses na hatimaye walimfungulia kesi mahakamani. Hata hivyo, baada ya Duale kuzungumza na wakili wa familia ya Sozigwa, aliambiwa ukweli kuwa hiyo nyumba ina utata wa wanafamilia hali iliyomsababishia Duale mshtuko hadi kupooza. “Huyu Duale alizungumza na wakili wetu, akaambiwa ukweli kuwa asinunue hiyo nyumba kwa kuwa haina hati na alipoonyeshwa hati halisi alishtuka na kupata kiharusi kwa sababu alikuwa ameshalipa fedha zote,” alisema Moses. Akiendelea kusimulia, Moses alisema mauzo ya nyumba hiyo yana utata na kuna dalili ya rushwa kwani yameidhinishwa na baraza la ardhi la Wilaya ya Temeke ambalo kwa kawaida, lina haki ya kuidhinisha mauzo ya nyumba yenye thamani ya Sh50 milioni na chini ya hapo, wakati thamani halisi ya nyumba hiyo ni Sh900 milioni. “Tunashangazwa na kitendo cha mama kuuza nyumba hiyo kwa Sh600 milioni wakati tathmini iliyofanywa mwaka 2010 ilionyesha kuwa ina thamani ya Sh900 milioni,” alisema Moses. Moses ambaye alizungumza kwa niaba ya ndugu zake watatu, Salome, Irene na Ephata alisema licha ya mama yao kuuza nyumba kwa mamilioni ya fedha lakini alikataa kusaidia kutoa fedha za kumpeleka baba yao nchini Finland kwa matibabu. “Ilitubidi kutembeza bakuli hadi kwa Rais Jakaya Kikwete ili tupate msaada wa matibabu ya mzee,” alisema. Mwananchi lilizungumza na Kuga ambaye alisema anawashangaa watoto wake kwa kushindwa kujua sheria zinavyofanya kazi na kuanza kumrushia tuhuma zisizo na ukweli kuwa ameuza nyumba kwa ujanja. “Hii kesi imeenda mahakamani  hadi mahakama kuu na nimeshinda mara tatu, lakini hawa wanaona kuwa wao ndiyo wana haki ya nyumba ambayo mimi na baba yao tuliijenga, wanakata rufaa kila siku,” alisema. Alieleza pia sababu za kuishi na Sozigwa licha ya kuwa walitengana kwa zaidi ya miaka 34. Alisema baada ya kuona hali ya mumewe huyo siyo ya kuridhisha aliamua kurejea kumtunza na siyo kwa ajili ya nyumba. “Nilimhurumia mzee nikaamua kuishi naye ili nimlee na ndiyo hapo tulipokubaliana naye tuiuze nyumba,” alisema. Kuga ambaye aliwahi kugombea ubunge wa Temeke kwa tiketi ya DP mwaka 1995, alisema watoto wake hao walifikia hatua ya kuficha hati halisi ya nyumba hiyo ili kuzuia uuzwaji. Lakini hata hivyo, Kuga alisema yeye na wakili wake walitoa matangazo kwenye magazeti kuwa hati hiyo imepotea ili kupata kibali kutengeneza hati mpya ili waweze kuiuza nyumba hiyo. “Hali ya baba yao ni mbaya lakini naona na hawa watoto hali yao ni mbaya zaidi kwa sababu hawajui kitu wanachokifanya; nyumba ni yetu mimi na mzee wao kinawauma nini? Alihoji. Kadhalika Kuga alisema mpaka sasa Duale tayari ana hati na ameshakuwa mmiliki kamili wa nyumba hiyo. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Warioba: CCM ina kazi ngumu kumpata mgombea urais

$
0
0

Dar es Salaam. Waziri Mkuu wa zamani, Jaji Joseph Warioba amesema CCM inakabiliwa na kazi ngumu ya kupata mgombea wa urais atakayepeperusha bendera ya chama hicho kwenye uchaguzi wa mwaka huu, akionya kuwa makundi ya urais yasipomalizwa yanaweza kufika hadi ngazi ya kata. Makada 38 wamejitokeza kuomba ridhaa ya chama hicho tawala ya kugombea urais katika kipindi ambacho kuna ongezeko kubwa la nguvu ya vyama vya upinzani, huku vyama vinne vikiwa vimeamua kusimamisha mgombea mmoja. Tayari vikao vya kujadili jinsi ya kumpata mteule wa kupeperusha bendera ya chama hicho vimeshaanza kwa wenyekiti na makamu wao kukutana na jana Kamati Kuu ilikuwa inakutana mjini Dodoma. Akiangalia hali hiyo, Jaji Warioba aliiambia Mwananchi jana kuwa chama hicho tawala kinatakiwa kuwa makini katika mchakato huo, kwa maelezo kuwa unaweza kuacha majeraha makubwa kutokana na makundi yaliyoibuka. “CCM inakabiliwa na wakati mgumu wa kupitisha jina la mgombea urais kutokana na waliojitokeza kuwania nafasi hiyo kufikia 38, na mpaka sasa imekuwa ni vigumu kutabiri atakayepitishwa, jambo ambalo halikujitokeza wakati wa upitishwaji wa mgombea urais wa chama hicho mwaka 1995 na 2005,” alisema Jaji Warioba, ambaye alikuwa mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Alisema kila unapofika Uchaguzi Mkuu kunakuwa na changamoto zake, lakini mwaka huu CCM inakabiliwa na changamoto kubwa zaidi kwa sababu uchaguzi huo utamleta rais mpya na mwenyekiti mpya wa chama hicho. Alisema jambo la kwanza lililotokea katika mchakato wa kumpata mgombea urais litakalokifanya chama hicho kuwa na wakati mgumu ni kitendo cha baadhi ya wagombea kueleza sera zao, wakati wakijua wazi kuwa sera za CCM ziko kwenye ilani yake ya uchaguzi. “Waliotangaza nia wamekuwa wakieleza sera zao na ukiwasikiliza unaona kama walikuwa wagombea binafsi hivi kwa sababu CCM ina sera, wanayo ilani ambayo ipo tayari na yeyote atakayepeperusha bendera ya CCM lazima ajikite kwenye ilani ya chama,” alisema jaji Warioba. “Kama mtu ametangaza sera na vipaumbele vyake na havifanani na vipaumbele vya ilani ya chama unafanyaje? Ni mtihani mwingine huo.” Alisema jambo la pili ni kukiukwa kwa utaratibu uliowekwa na chama hicho kwamba yeyote anayehusika kwenye ngazi ya maamuzi, asimdhamini mgombea yeyote wa urais, huku akiwatolea mfano wajumbe wote wa mkutano mkuu wa chama hicho ambao ndio humchagua mgombea urais wa chama hicho. “Nimeambiwa kwamba wajumbe wa mkutano mkuu walikatazwa kudhamini wagombea, lakini tulivyoona ni kwamba viongozi wengi wameonyesha waziwazi wapo kundi gani, wapo waliojitokeza na kusema na wengine hawakusema lakini wanajulikana wanamuunga mkono mgombea gani,” alisema. “Hawa ndio watakwenda kuchuja, sasa hapa itakuwa kazi ngumu na inawezekana kukawa na mgongano wa maslahi na hilo lisipoangaliwa linaweza kufanya mchujo ukaonekana kuwa haukuwa wa haki. Jambo hili linatakiwa kuangaliwa na hasa kwa kuwa kuna makundi.” Alisema makundi yaliyoibuka ndani ya chama hicho yanaweza kuifanya CCM ikalegalega na hasa kama wengine watafikiri utaratibu uliotumika wa kumpata mgombea haukuwa wa haki. “Hali hiyo ikitokea itakuwa ngumu kuyarudisha makundi hayo ili kuwa kitu kimoja,” alionya Jaji Warioba ambaye pia aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. “Katika siasa chama ndiyo muhimu na kisipokuwa imara, mgombea yeyote wa chama husika hataweza kuwa na nguvu sana. Nadhani itasababisha matatizo na si katika urais tu, haya makundi yasipopatana yakaendelea na uhasama itakwenda mpaka kwenye majimbo na kata,” alisema. Alisema mwaka huu ni wa ushindani na kama CCM isipochukua tahadhari katika kumpata mgombea, chama hicho kitakumbana na wakati mgumu. Kamati Kuu ya CCM itakutana Julai 9 kufanya mchujo na Julai 10 Halmashauri Kuu itakutana kupanga ajenda za Mkutano Mkuu ambao utafanyika Julai 11-12 kwa ajili ya kumchagua mgombea urais. Kamati Kuu, ambayo ndiyo msingi wa maamuzi yote, inaundwa na mwenyekiti, ambaye ni Rais Jakaya Kikwete; mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein; Makamu mwenyekiti, Philip Mangula; katibu mkuu, Abdulrahman Kinana; makamu wa Rais, Dk Mohamed Ghalib Bilal; Waziri Mkuu, Mizengo Pinda; Spika Anne Makinda na Balozi Seif Ali Iddi. Wengine ni Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Amir Kificho; Rajab Luhwavi, Vuai Ali Vuai, Nape Nnauye, Mohamed Seif Khatibu, Zakhia Meghji, Asha Rose- Migiro, Sophia Simba, Sadifa Juma Khamis, Abdallah Bulembo, Jenister Mhagama, William Lukuvi. Wengine ni Steven Wasira, Dk Emmanuel Nchimbi, Pindi Chana, Jerry Silaa, Adam Kimbisa, Shamsi Vuai Nahodha, Dk Hussein Mwinyi, Maua Daftari, Samia Suluhu, Dk Salim Ahmed Salim, Makame Mbarawa na Hadija Abood. Msekwa anena Wakati Jaji Warioba akitafakari mustakabali wa CCM, makamu mwenyekiti wa zamani wa chama hicho, Pius Msekwa amesema ukiukwaji wa kanuni na taratibu za uchaguzi itakuwa ni moja ya mambo mawili makubwa yatakayoangaliwa kwenye mchujo wa wagombea. Mbali na ukiukwaji huo wa taratibu, watatumia vigezo 13 vilivyowekwa na chama hicho kumpata Rais wa Serikali ya Awamu ya tano na mwenyekiti wa chama hicho. Tayari baraza hilo linaloongozwa na Rais wa Serikali ya Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi limeripotiwa kuanza kazi ya uchambuzi na litawasilisha taarifa yake kwa Kamati Kuu . Wajumbe wengine wa baraza hilo la wazee ni Rais wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, marais wa zamani wa Zanzibar Aman Abeid Karume na Dk Salmin Amour. Jana, Msekwa ambaye amewahi kuwa makamu mwenyekiti wa CCM-Bara, alisema kazi hiyo itafanywa kwa umakini mkubwa kwa kuzingatia mambo hayo mawili. “Sifa zimeandikwa kwenye kanuni zetu za chama na zipo 13. Hizo ndizo zitakuwa kipimo cha wagombea katika vikao na watachujwa kwa kuzingatia hilo. Ni lazima kutazama kama mgombea ana sifa hizo,” alisema. “Pili, tunatazama kama mgombea amekiuka masharti yoyote ya kanuni zetu maana unaweza kuwa na sifa lakini ukawa umekiuka masharti.” Alisema mambo hayo mawili ndiyo yatakayotumika na hakuna kigezo kingine chochote kitakachomfanya mtu kupata au kukosa nafasi. Msekwa alikumbushia makada wa chama hicho waliowahi kukumbana na adhabu baada ya kukiuka masharti ya kanuni akisema: “Nadhani unakumbuka wapo waliowahi kusimamishwa kutokana na kukiuka masharti ya kanuni baada ya kuanza kampeni mapema. Kwa sasa wameshafunguliwa.” Makada waliopewa ‘adhabu ya kifungo’ cha mwaka mmoja kutokana na kujihusisha na kampeni za urais kabla ya wakati ni mawaziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa na Frederick Sumaye, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na Waziri wa Kilimo na Ushirika, Steven Wasira. Wengine ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Risasi zarindima BVR, mkutano ZEC wavunjika

$
0
0

Zanzibar. Wakati watu watano wakijeruhiwa, wawili kwa kupigwa risasi, kwenye uandikishaji wa wapigakura eneo la Makunduchi, mkutano baina ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar na wadau umevunjika kutokana na mzozo wa mgwanyo wa majimbo. Vurugu hizo zimetokea baada ya watu waliokuwa wamekusanyika katika Msikiti wa Kubini kwa madhumuni ya kupinga kazi hiyo ya uboreshaji wa Daftari la Wapigakura wakituhumu kuwapo kwa mamluki waliokuwa wakiandikishwa, lakini wakajikuta wakivamiwa na kundi la askari wasiokuwa na sare ambao walikuwa na silaha za moto. Waliojeruhiwa kwa risasi ni Kheri Makame Hassan (42) na Ramadhani Hija Hassan (29) wote wakazi wa Makunduchi wakati Ali Seif Issa (38), Ali Hassa Hassan (70) kutoka Paje akiwa amepigwa kwa magongo na nondo na kuumia vibaya miguuni, na Hassan Ali Ameir (43). Wakizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti hospitalini hapo, majeruhi wao walisema walikuwa katika kituo cha Nganani, Shehia ya Nganani Kusini Unguja ndipo walipokuja watu waliovaa vinyago na kuwaamuru waondoke eneo hilo wakati uandikishaji ukiendelea. “Ilikuja gari na watu waliojifunika nyuso zao wakatuambia tuondoke na sisi tukakataa kwa sababu tulikuwa tunazuia kuandikishwa mamluki katika eneo letu. Baada ya kubishana pale wakaenda kuchukua gari nyingine wakaanza kutupiga,” alisema Kheri ambaye amepigwa risasi ya pajani. “Watu waliojifunika nyuso walikuja mara mbili na kuondoka kabla ya kufanya shambulio na kufanikiwa kuondoka katika eneo la tukio la Nganani kwa kutumia magari mawili,’ alisema Faki huku akilalamika kusikia maumivu. Shuhuda wa tukio hilo, Ameir Mussa, mkazi wa Makunduchi, alisema kwamba waliamua kukusanyika eneo la msikiti wakitafakari jinsi ya kuzuia uandikishaji wa wapigakura mamluki, ambao ni pamoja na walio na umri mdogo. “Lilikuja kundi la watu mara mbili na kuondoka. Walikiwa wamefunika nyuso zao na waliporudi kwa mara ya mwisho walitushambulia kwa kutumia silaha za kienyeji na baadaye kufyatua risasi za moto na kujeruhi watu wawili,” alisema Mzee Ameir. Daktari wa zamu wa Hospitali ya Al Rahma, Seif Suleiman alithibitisha kupokea majeruhi na kusema kwamba katika hatua za awali wanazuia damu kuvuja kutoka kwenye majeraha. Alisema wanaendelea na vipimo ili kujua majeraha hayo yamesababishwa na nini. “Tumewafanyia x-ray ili kujua majeraha yao yanatokana na nini lakini yanaonesha wazi kuwa ni majeraha kama ya risasi kwa kuwa risasi jeraha lake linakuwa ni kitobo kidogo inapoingia lakini kitobo kikubwa inapotokea risasi.” Dk Suleiman alisema majeruhi hao wanaendelea vizuri baada ya kutibiwa na wengine wataruhusiwa watakapopata nafuu. “Wapo walioumia sana hao wataendelea kuwepo hospitali kwa sababu wametokwa damu nyingi sana na kutoka Makunduchi hadi Mjini ni mbali kwa hivyo wanahitaji kupumzishwa kwanza hadi hapo watakapopata nafuu,” aliongeza Dk Suleiman. Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kusini Unguja, Juma Saadi alisema kuwa katika mkoa wake kuna uandikishaji wananchi kuwaingiza kwenye Daftari la Wapigakura, lakini hana taarifa za watu kupigwa risasi na kwamba anachojua ni risasi hizo kupigwa hewani na hivyo hazijajeruhi mtu. “Taarifa nilizonazo ni kwamba polisi wamerusha risasi juu kwa bahati mbaya wakati wakijitayarisha kuweka sawa vifaa vyao,” alisema Kamanda Saad. Hata hivyo, Kamanda Saad aliahidi polisi kufanya upelelezi wa kina ili kujua ni kina nani wanahusika na urushaji wa risasi hizo ambazo zimewajeruhi wananchi waliokuwepo katika eneo hilo la uandikishaji wapigakura. Majeruhi wao walipelekwa Hospitali ya Al Rahma na kupatiwa matibabu na habari zinasema hali ya mmoja wao si nzuri na amehamishiwa Hospitali ya Mnazi Mmoja kwa matibabu zaidi. Wakati huohuo, kikao baina ya ZEC, vyama vya siasa na wadau kilichokuwa kinafanyika jana kisiwani hapa, kilivunjika jana baada ya tume kushindwa kuwasilisha ripoti ya mgawanyo mpya wa majimbo ya uchaguzi. Uchaguzi Mkuu umepangwa kufanyika Oktoba 25, lakini hadi sasa ZEC haijaweza kutangaza majimbo mapya, jambo lililozua mzozo kwenye kikao hicho kilichofanyika Hoteli ya Bwawani. Kikao hicho kilivujika baada ya mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salum Jecha kumaliza kutoa utangulizi kuhusu hatua zilizofikiwa katika kazi ya kutayarisha mipaka ya majimbo. Alisema kimsingi ZEC tayari imeshamaliza kazi ya kufanya mapitio ya mipaka ya majimbo ya Zanzibar na kwamba wanatarajia kutoa taarifa rasmi wiki ijayo na kuwataka wadau wa uchaguzi kuendelea kuwa na subira wakati wakikamilisha kazi hiyo. Jecha alisema kwamba kazi ya kupitia mipaka ya majimbo ilianza kufanyika Juni 9 mwaka jana na kuwapa nafasi wadau wa uchaguzi kutoa maoni yao na hatua iliyobakia ni kutangaza mipaka ya majimbo. Hata hivyo, mwenyekiti wa chama cha AFP, Said Soud alisema kwamba anashangazwa na ZEC kushindwa kukamilisha kwa wakati mwafaka kazi hiyo na badala yake kuendelea kutoa ahadi. “Wakati umefika wa kumshauri Rais wa Zanzibar kuvunja uongozi wa ZEC kwa sababu wanaonekana bado wanavutana na ndiyo maana wanapiga danadana katika kutoa taarifa ya ugawaji wa mipaka ya majimbo ya uchaguzi ya Zanzibar,” alisema Soud Mwakilishi wa CCM, Rashid Ali alisema kitendo cha ZEC kuendelea kuchechemea kutoa taarifa ya mabadiliko ya mipaka kimeendelea kuathiri vyama vya siasa kwa wagombea kushindwa kuanza kufanya matayarisho ya wagombea ubunge na uwakilishi katika majimbo ya Unguja na Pemba. “Kama majimbo ya uchaguzi ni ya wananchi, kwa nini ZEC mnashindwa kufanya kazi ya kupitia majimbo kwa muda muafaka wakati nyie ndiyo wasimamizi wa uchaguzi?” alihoji. Mkurugenzi wa uenezi na mawasiliano ya umma wa CUF, Ismail Jussa Ladhu alisema wameshachoshwa kudanganywa na ZEC kuhusu taarifa ya mapitio ya mipaka ya majimbo ya uchaguzi, akielezea kuwa kitendo hicho ni usanii. Alisema kwamba ZEC walitoa ahadi ya kutoa taarifa ya mipaka ya majimbo ifikapo Machi mwaka Huu, lakini walishindwa na kuendelea kutoa ahadi nyigine bila ya utekelezaji wake kuonekana, jambo ambalo halionyeshi umakini wa utendaji kazi wa tume hiyo. Akizungumzia mkasa huo katibu mkuu wa Tadea alisema kwamba inasikitisha muda wa uchaguzi umekaribia lakini hadi sasa hawajui mgawanyo wa majimbo. Miongoni mwa wadau waliyoshiriki Kikao hicho ni vyama vya siasa, na asasi za kiraia, vikosi vya ulinzi na taasisi za Serikali. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Dr Shein Apitishwa Kuwa Mgombea Urais wa Zanzibar Kupitia CCM.

$
0
0

Kamati kuu maalum ya chama cha mapinduzi Zanzibar kwa kauli moja imempitisha Dr Ali Mohamed Shein kuwa mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama cha mapinduzi. Hatua hiyo imefikiwa baada ya wajumbe wa NEC wa Zanzibar wanounda kamati maalum ya Zanzibar kukutana hapa Zanzibar katika ofisi kuu ya CCM na kuamua kumuidhinisha Dr Shein kugombea tena  kiti hicho cha urais baada ya wajumbe karibu 102  ambao ni aslimia 83  kuridhia Dr Shein agombee. Awali Dr Shein ambaye ni makamu mwenyekiti wa CCM Zanzibar alilazimika kuondoka ndani ya kikao ili ijadaliwe na wanachama hao ambapo kiti hicho kilishikwa kwa muda na Dr Mohamed Gahribu Bilali makamu wa rais, ambapo baadaye akizumgumza na wanaccm hao waliokubali Dr Shein aliwahidi wanachama wa CCM kuwa  uamuzi wake uko palepale wa kutekeleza ilani ya CCM ya kuitumikia Zanzibar. Katika hatua nyengine naibu katibu mkuu wa CCM Zanzibar akizungumza baada ya kikao hicho alisema CCM haiwezi kupinga au kukubali suala la majimbo,wao wanasubiri maamuzi ya tume na wako tayari kwa umauzi wowote utakaotolewa na tume ya uchaguzi ambayo inatarajiwa kutangaza majimbo mapya leo asubuhi. Kupitishwa kwa Dr Shein kugombea urais wa Zanzibar na kamati maalum ni hatua ya kwanza na sasa shuguhli yote inahamia Dodoma ambapo jina la Dr Shein litajadiliwa na kamati kuu na baadaye kutakiwa kuidhinishwa na kupitishwa na halmashuri kuu ya CCM, nafasi ya urais wa Zanzibar inaamuliwa na NEC na siyo na mkutano mkuu waccm. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Rose Mhando Apigwa Pingu Dodoma……Asafirishwa Kwenda Dar

$
0
0

Kufuatia skendo ya utapeli inayoendelea kumwandama mwimbaji wa nyimbo za Injili Bongo, Rose Muhando anadaiwa kupigwa pingu mkoani Dodoma, baadaye akasafirishwa hadi Dar kwa msimamizi wa kazi zake, Alex Msama, kwa lengo la kumlipia deni alilokuwa akidaiwa. Habari kutoka kwa chanzo zimeeleza kwamba, hivi karibuni, Rose alilipwa Sh. milioni 3 kwa ajili ya shoo huko Makambako mkoani Njombe na matangazo yakafanyika lakini hakutokea.   Ikadaiwa kuwa, wakati matangazo ya shoo yakiendelea, mtu mwingine aliyekuwa akimdai Sh. milioni 3.5 (pia alichukua fedha kwa shoo siku za nyuma) alikwenda Makambako kwa lengo la kumsubiri Rose ili amnase, lakini hakutokea.   Chanzo hicho kiliendelea kumwaga ‘unyunyuzi’ kuwa, wawili hao waliripoti ishu ya Rose, Kituo cha Polisi Makambako ambapo polisi walifunga safari kumfuata Dodoma.   Sosi huyo alisema kuwa, Rose alikamatwa Juni 27, mwaka huu na kuswekwa rumande Kituo Kikuu cha Polisi, Dodoma tayari kwa kupelekwa mahakamani.    Imedaiwa kuwa, kigogo mmoja wa serikali mkoani humo (jina lipo) aliwaambia polisi wampigie simu Msama na kumweleza kisanga hicho ili ikibidi yeye amlipie deni hilo kwa sababu anamsimamia kazi zake.   “Msama alikubali kwa sharti kwamba, kwa sababu ana kazi ya kufanya na Rose hivyo asafirishwe hadi Dar amlimpie, yeye na Rose watakatana kwenye kazi.   “Rose alisafirishwa Juni 29, mwaka huu akiwa chini ya ulinzi wa askari wawili. Mmoja wa kike ambaye alilala naye chumba kimoja hotelini. Kesho yake wakaenda ofisini kwa Msama, Block 41, Kinondoni, akalipa milioni sita na laki tano keshi,” kilisema chanzo. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Utafiti Urais 2015: Lowassa Aongoza Mbio za Urais………Dr Slaa Ashika Nafasi ya Pili

$
0
0

Zikiwa zimebakia siku sita kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumpata mgombea wake wa urais katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu, kura ya maoni iliyoendeshwa na Mpango wa Utafiti na Elimu ya Demokrasia (REDET) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, inamweka kileleni Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, kuwa changuo la kwanza la wengi kwa kujipatia asilimia 27.0 ndani ya chama hicho. Wakati Lowassa akiwafunika watia nia wenzake ndani ya CCM, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa, anawafunika wenzake kwenye Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) akiwa changuo la wengi kwa asilimia 23.1.   REDET wamesema kuwa matokeo ya utafiti huo yanaweza kuchukuliwa kwa ujumla wake kama maoni ya Watanzania endapo masuala yaliyoulizwa uchaguzi ungefanyika katika kipindi cha utafiti. “Sampuli iliyotumika katika utafiti huu kwa kiwango cha kutosha ni wakilishi na ina akisi hali halisi ya Watanzania,”  imesisitiza ripoti hiyo iliyojatwa kuwa ni maoni ya wananchi kuhusu Uchaguzi Mkuu ujao wa Oktoba 2015, mwaka huu. Katika utitiri wa watia nia ndani ya CCM, kati ya wahojiwa 1,250 waliohojiwa, Lowassa alipigiwa kura na watu 338, wakati Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, akipata asilimia 8.2 akichaguliwa na watu 103. Utafiti wa REDET ulifanyika katika wilaya moja moja kwenye mikoa 25 ya Tanzania Bara baada ya wahojaji kukataliwa ruhusa ya kufanya utafiti wao katika mikoa mitano ya Zanzibar. Utafiti huo uliokuwa umedhaminiwa na kampuni ya Business Times Limited, ulifanyika kati ya Juni 23-26, mwaka huu na kila wilaya ilikuwa na wahojiwa 50. Kwa upande wa CCM watia nia wengine ni Mizengo Pinda nafasi ya tatu akiwa na asilimia 7.2 akichaguliwa na watu 90; John Magufuli nafasi ya nne akipata asilimia 6.6 akipigiwa kura na watu 83 na Charles Makongoro Nyerere nafasi ya tano akipigiwa kura na watu 54. Wengine ni Mark Mwandosya nafasi ya sita akipata asilimia 3.1 akichaguliwa na watu 39; Dk. Harrison Mwakyembe nafasi ya saba akiwa na asilimia 1.4 akichanguliwa na watu 18; Frederick Sumaye nafasi ya nane akipata asilimia 1.4 akichaguliwa na watu 17; nafasi ya tisa imekamatwa na Jaji Augustino Ramadhani akiwa na asilimia 1.2 akichaguliwa na watu 15 na nafasi ya 10 amekamata Mwigulu Nchemba akiwa na asilimia 1.0 akichaguliwa na watu 13. Wengine na idadi ya waliowachagua na asilimia zao kwenye mabano ni January Makamba nafasi ya 11 (asilimia 0.8, watu 10); Dk. Asha-Rose Migiro nafasi ya 12 (asilimia 0.7, watu tisa); Samuel Sitta nafasi 13 (asilimia 0.6. watu wanane); Lazaro Nyalandu nafasi ya 14 (asilimia 0.4, watu watano). Pia wamo Prof. Sospeter Muhongo nafasi ya 15 (asilimia 0.4, watu watano); Balozi Amina Salum Ali nafasi ya 16 (asilimia 0.2, watu wawili); Dk. Mohammed Gharib Bilal nafasi ya 17 (asilimia 0.2, watu watatu); Stephen Wasira nafasi ya 18 (asilimia 0.2, watu 3) na William Ngeleja nafasi ya 19 (asilimia 0.2, watu wawili). Wengine ni Balozi Ally Karume nafasi ya 20 (asilimia 0.1, mtu mmoja); Amos Siyantemi nafasi ya 21 (asilimia 0.1, mtu mmoja); Joseph Chagama nafasi ya 22 (asilimia 0.1, mtu mmoja); na Mwele Malecela nafasi ya 23 (asilimia 0.1, mtu mmoja). Katika kura hiyo, watia nia 14 ambao wamejitosa kwenye urais kupitia CCM hawakutajwa kabisa na watoa maoni ambao ni Balozi Augustine Mahiga; Boniphace Ndengo; Eldophonce Bihelo; Godwin Mwaipopo; Dk. Hamis Kigwangalla; Dk. Hans Kitine; Joseph Chagana; Leons Mulenda; Luaga Mpina; Maliki Marupu; Mathias Chikawe; Monica Mbega; Titus Kamani na Balozi Patrick Chokala. Kwenye kundi la Ukawa, namba mbili amechukua Prof. Ibrahim Lipumba akiwa na asilimia 13.6 akichaguliwa na watu 170; Freeman Mbowe ameshika nafasi ya tatu akiwa na asilimia 7.2 akichaguliwa na watu 90; James Mbatia amekamata nafasi ya nne akiwa na asilimia 3.2 akichaguliwa na watu 40; Emmanuel Makaidi akishikilia nafasi ya tano kwa asilimia 0.6 akichaguliwa na watu 8, huku George Kahangwa akishika nafasi ya sita kwa asilimia 0.2 akichaguliwa na watu wawili. SWALI LA MSINGI Swali la msingi lililokuwa linaulizwa lilisema: “Kama wewe leo ungeshirikishwa katika mchakato wa uteuzi wa mgombea urais kwa tiketi ya CCM, kati ya wanachama wake 37 waliokwishajitokeza, ungemchagua nani apeperushe bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Oktoba 2015?” Pia swali kwa Ukawa lilikuwa: “Kama wewe leo ungeshirikishwa katika mchakato wa uteuzi wa mgombea urais kwa tiketi ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kati ya wanachama wake waliokwishakutangaza nia na wanaotarajia kutangaza nia ungemchagua nani apeperushe bendera ya Ukawa katika uchaguzi mkuu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Oktoba 2015?”  Ripoti ya REDET imesema kuwa kwa maswali yote, mhoji alitakiwa kutomtajia majina mhojiwa, bali mhojiwa aliombwa ataje jina alilonalo kichwani mwake. REDET imesema kuwa katika utafiti wake ilikusudia kupata maoni ya wananchi katika maeneo matatu; mosi, kupata maoni ya wahojiwa kuhusu wanachama wa CCM wanaoomba kuteuliwa kuwania nafasi ya urais kwa tiketi ya chama hicho; mbili, kupata maoni ya wananchi kuhusu wanachama wa vyama vinavyounda Ukawa ambao wamejitokeza au wanafikiriwa kuwania nafasi ya urais chini ya mwavuli wa Ukawa na tatu, kupata maoni ya wahojiwa kuhusu wanachama wa vyama vingine vya upinzani vilivyo nje ya Ukawa wanaofikiriwa kwania nafasi ya urais. Katika kundi la vyama ambavyo havipo Ukawa, Zitto Kabwe ameongoza kwa asilimia 8.5 akichaguliwa na watu 106, Chama cha Demokrasia Makini kimepata asilimia moja kilichaguliwa na watu 13, John Cheyo ameibuka nafasi ya tatu akiwa na asilimia 0.9 akichaguliwa na watu 12 na Augustine Mrema nafasi ya nne akiwa na asilimia 0.7 akichaguliwa na watu wanane.  Wengine ni Chama cha ADC nafasi ya tano kikiwa na asilimia 0.5 kikichaguliwa na watu sita na nafasi ya sita yupo Christopher Mtikila akiwa na asilimia 0.5 akichaguliwa na watu sita pia. WILAYA ZA KURA YA MAONI Wilaya ambazo kura ya maoni iliendeshwa ni Longido, Temeke, Dodoma Manispaa, Mbogwe, Kilolo, Muleba, Mlele, Ujiji Kigoma, Moshi Manispaa, Lindi, Hanang, Bunda, Rungwe, Morogoro Manispaa, na Msasi. Nyingine ni Ilemela Manispaa, Ludewa, Kisarawe, Kalambo, Namtumbo, Kahama, Itilima, Singida, Tabora Manispaa na Muheza.  Ambako ruhusa haikupatikana ni Micheweni, Kaskazini B, Mkoani, Kusini na Mjini  A. VIJANA ZAIDI WAJITOKEZA Katika utafiti huo ambao ulitumia mfumo wa sampuli nasibu (random sampling), vijana wengi zaidi walitoa maoni yao. Wahojiwa 334 sawa na asilimia 26.7 walikuwa kati ya umri wa miaka 36 – 45 na wengine 201 kati ya miaka 18 – 25 wakiwa ni asilimia 16.1. Wahojiwa wachache yaani zaidi miaka 66 walikuwa ni 70 sawa na asilimia 5.6. Wanawake katika wahojiwa walikuwa 626 sawa na asilimia 501, huku wanaume wakiwa ni 624 sawa na asilimia 49.9. Asilimia 30 ya wahojiwa wote walitoka mijini, huku asilimia 70 wakitoka maeneo ya vijijini. VIPAUMBE SERIKALI AWAMU YA TANO REDET wanasema kuwa wahojiwa walitakiwa kutaja kipaumbele kimoja tu na mlolongo uliopatikana ni elimu asilimia 23.8 iliyotajwa na watu 298; kilimo asilimia 14 watu 175, ajira asilimia 12 watu 150, afya asilimia 9.9 watu 124, kupambana na rushwa asilimia 6.4 watu 80 na maji asilimia 5.4 watu 68. Nyingine ni barabara iliyoshika nafasi ya saba iliyopata asilimia 3.4 ikitajwa na watu 43, viwanda asilimia 3.3 ikitajwa na watu 41 na mikopo na mitaji asilimia 2.6 ikitajwa na watu 33. Vipaumbelea vingine na asilimia na idadi ya waliotaja kwenye mabano ni umeme (asilimia 2.2, watu 28), kukomesha migogoro ya ardhi (asilimia 1.5, watu 19), ujenzi wa makazi/ nyumba bora (asilimia 0.6, watu 7), demokrasia (asilimia 0.6, watu 8), katiba inayopendekezwa (asilimia 0.3, watu watu 4) na muungano (asilimia 0.1, mtu mmoja).  FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat


Rais Kikwete Awakemea Wanaotumia fedha ili kupata madaraka

$
0
0

RAIS Jakaya Kikwete, amewataka viongozi wa dini nchini kutowapa mwanya wanasiasa wenye dhamira ovu ya kuwafarakanisha Watanzania bali waendelee kukemea matumizi mabaya ya fedha, rushwa na hujuma katika Uchaguzi Mkuu hasa kipindi hiki. Alisema ipo haja ya viongozi hao kuendelea kuwakemea wanasiasa  wanaopenda madaraka kwa gharama yoyote wakitumia fedha kununua ushindi au ubaguzi wa rangi, kabila, dini, kuwabagua wapinzani wao na kujijenga zaidi kisiasa.  Rais Kikwete aliyasema hayo jana katika Maadhimisho ya Miaka 125 ya Injili katika Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), yaliyofanyika katika Viwanja vya Mbuyukenda, mkoani Tanga. Aliwaomba viongozi wa dini na wananchi, wasiwasikilize wanasiasa wenye dhamira ovu wala kuwaendekeza kwani mchezo wao ni mauti ya Watanzania hivyo wawakatalie kwa macho makavu. Alisema si vyema kukaa kimya dhidi ya watu wanaokiuka maadili na kuchochea mifarakano katika Taifa kwani watu hao si wema bali wataifikisha nchi pabaya hivyo wasiruhusiwe kuchezea dini zetu ambazo ni mhimili muhimu wa amani yetu tofauti na ukabila. “Tusikubali kumchukiza Mungu akatukasirikia na kutuadhibu kwa jambo ambalo liko ndani ya uwezo wetu kulizuia lisitokee, mambo yakiharibika hatuwezi kumlaumu mtu mwingine yeyote bali sisi wenyewe.  “Katu hatuwezi kusema ni mapenzi ya Mungu bali itakuwa ni makosa yetu wenyewe, nawaomba viongozi wa dini mlisaidie Taifa letu, limeni mraba wenu vizuri nasi tulime wetu, msiwape nafasi viongozi wa siasa na hata wa dini kutumia majukwaa ya dini kuendeleza maslahi yao ya kisiasa hasa kupandikiza chuki katika jamii,” alisema. Rais Kikwete aliongeza kuwa, Serikali inawategemea viongozi wa dini wasiwe sehemu ya makundi ya wagombea au vyama vya siasa bali wanapaswa kuwa pande zote ili waweze kufanya vizuri kazi yao ya kuliponya Taifa kama kutatokea matatizo. Aliongeza kuwa, Serikali haitegemei viongozi wa dini wawapangie waumini wao vyama au viongozi wa kuwachagua bali wawahimize na kuwakumbusha waweze kutumia haki na wajibu wao vizuri. “Muwakumbushe mambo muhimu matatu, kwanza kujiandikisha, pili, kujitokeza kwenda kupiga kura, tatu kuchagua viongozi wazuri wasio waovu, wasiofanana na uovu na kuukaribia uovu, watakaosukuma mbele gurudumu la maendeleo na kujali maslahi mapana ya jamii husika na nchi yetu,” alisema Rais Kikwete. Aliwaomba waendelee kuiombea Tanzania iendelee kuwa ya amani na utulivu ili watu wake wadumishe upendo na mshikamano miongoni mwao na kuombea Uchaguzi Mkuu ujao uwe salama ili Taifa lipate viongozi wazuri, liendelee kuwa tulivu kabla, baada ya uchaguzi. Alisema historia inaonesha kuwa, katika nchi nyingi za Afrika wanasiasa hutumia kupindi cha uchaguzi kufanya maasi hivyo uadilifu na tahadhari kubwa inahitajika. Kwa upande wake, Askofu wa Kanisa hilo Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dkt. Stephen Munga, alisema ili Taifa liweze kuvuka kipindi cha uchaguzi salama, Uchaguzi Mkuu ufuate misingi yote iliyowekwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), ili kuwapa uhuru wananchi waweze kuchagua viongozi wanaowataka. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Ugiriki wapiga kura ya Hapana

$
0
0

Maelfu ya raia wa Ugirik usiku wa leo wametawanyika katika mitaa ya mjini Anthens karibu na jengo la bunge, wakifurahia kura ya hapana waliyoipiga ambayo imeshinda kwa ya asilimia 60. Waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras,amesema matokeo hayo ya hapana, hayana nia ya kwenda kinyume na jumuiya ya Ulaya bali yataiongezea Ugiriki uwezo wa majadiliano zaidi kuhusiana na mzozo wa madeni. Tsipras ameongeza kuwa serikali ya Ugiriki iliitisha kura hiyo ya maoni ikiamini kuwa kura ya Hapana italeta makubaliano mazuri, pamoja na kwamba kuna onyo kutoka kwa viongozi wa ukanda wa Euro kuwa hatua hiyo itasababisha Ugiriki kuondolewa katika nchi wananchama wa ukanda huo. Naye Rais wa Bunge la Jumuiya ya Ulaya Martin Schulz amesema kuwa kura hiyo ya HAPANA inaiacha Ugiriki katika mazingira mabaya zaidi kuhusiana na mzozo wa madeni na vikwazo vya kimataifa. Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier anasema kwa matokeo hayo sasa umamuzi ni wa mahakama ya Ugiriki kwani wapiga kura wamepinga kwa nguvu zote masharti ya wakopeshaji wa kimataifa Matokeo haya yanasababisha kukubalika zaidi kwa Waziri mkuu wa Ugirik Alexis Tsipras japo kuwa pia anakuwa na wajibu mkubwa wa kukabiliana na mazingira yote ya kipindi hiki cha mpito kuhusiana na mzozo wa madeni. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Marekani bingwa kombe la Dunia wanawake

$
0
0

Marekani imeibuka mshindi wa Kombe la Dunia soka wanawake kwa kuichabanga Japan kwa bao 5 kwa 2. Katika fainali hii makubwa yaliweza jitokeza katika uwanja wa Vancouver mbele ya hamsini elfu mashabiki baada ya Wamarekani kufunga mabao manne kwa mfululizo katika dakika kumi na tano za mwanzo wa mchezo. Carli Lloyd alifanya hila mpaka muda mfupi baada ya mechi akapatiwa taji lai mchezaji bora wa mashindano. Hata hii ni mara ya tatu katika michuano ya Kombe la dunia ya timu ya Marekani ya wanawake kutokea hila hizi.Maafisa kutoka FIFA wameshutumu uongozi wa soka duniani kwa kupingwa na umati wa watu. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Power Circuit of a single (1) Phase Direct On Line DOL Electric Motor Controller – A basic industrial process automation control how to do guide

$
0
0

Further to the previously discussed electric motor controller with a three (3) phase Direct On Line (DOL) power circuit is the application of similar DOL power circuit for a single (1) phase small size AC electric motor. The electrical diagram on the right used in every electrical industry involving industrial process automation control technology shows a similar power circuit identical to the 3 phase DOL motor controller power circuit except for the distinguishable difference on the wiring connection of the circuit specifically intended to accommodate a 1 phase motor instead of a 3 phase motor. In the absence of single (1) phase motor controller devices, an available three (3) phase magnetic contactor and thermal overload relay can be used as well in a 1 phase circuit. You will notice from the presented diagram that the wiring configuration to the terminal of the three pole main contactor and thermal overload relay utilized all three terminals despite the common knowledge of a two line electricity flow path inherent with single phase circuits. This type of connection is done to achieve a complete current flow measurement to maintain a balance load current detection   from the 1 phase motor concentrated on the three poles of the thermal overload relay. Why? Because leaving out one terminal open for a 1 phase application would result in an imbalance distribution of load current detection on the 3 terminals of a 3 pole thermal overload relay. Since a three pole thermal overload relay is specifically designed to detect an equal three phase load current, then the application of an unequal load concentrated only on two terminals with one terminal open would eventually render an inaccurate current measurement resulting in an intermittent unnecessary tripping OFF of the thermal overload relay.  FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Mbunge Wa CHADEMA Ajivua Uanachama……Asema Kama CHADEMA Wanaubavu Wakalikomboe hilo Jimbo

$
0
0

MBUNGE wa Mpanda Mjini, Said Arfi, jana aliwaaga wapiga kura wake akiwaeleza kuwa uanachama wake Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) utakoma mara baada ya kuvunjwa kwa Bunge la 10 mjini Dodoma. Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Shule ya Msingi Kashato mjini hapa jana, Arfi, aliyekiwakilisha chama hicho kwa miaka 10 mfululizo, aliwaambia wananchi kuwa jimbo hilo litakuwa wazi wakati wowote wiki ijayo.    “Kama Chadema wana ubavu, waje walikomboe jimbo hili. Mimi ninaifahamu Chadema kuliko mtu yeyote mkoani Katavi kwani nilikuwa Makamu Mwenyekiti (Bara), na sasa nitamuunga mkono yeyote anayefaa kuwa mrithi wangu,”  alisema Arfi na kushangiliwa.    Mkutano huo uliohudhuriwa na umati mkubwa, ulikuwa chini ya ulinzi mkali wa polisi kutokana na kuzagaa kwa taarifa za kutaka kufanyiwa fujo kwa Mbunge huyo na watu wanaoaminika kuwa wafuasi wa Chadema.    Arfi alisema hatogombea tena Mpanda Mjini;  “Lakini nipo tayari kuvaa shati la kijani au la zambarau kumpigia debe mgombea yeyote katika jimbo hili. Ninawajua Chadema na kama wakiendelea kunifuatafuata, nitasema yote.”    Kauli hiyo ilitafsiriwa kuwa Arfi sasa atafanya kampeni akiwa CCM au ACT Wazalendo dhidi ya Chadema katika Jimbo la Mpanda Mjini, ambalo kabla yake halikuwahi kutawala na Mbunge mmoja kwa miaka 10 mfululizo.    Hii ni mara ya kwanza kwa Arfi kuweka hadharani mustakabali wake kisiasa, lakini kauli yake ya kuwa tayari kuvaa shati la kijana inakwenda tofauti na fununu zilizozagaa mjini hapa kuwa huenda akajiunga na ACT Wazalendo, chama kinachoongozwa na swahiba wake, Zitto Kabwe.    Ikumbukwe kuwa mara baada ya Chadema kutangaza kumvua nyadhifa zote Zitto takriban miaka miwili iliyopita, mara moja Arfi alitangaza kuajiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Kiunzi cha kwanza urais CCM kesho

$
0
0

Dodoma. Kamati ya Maadili na Usalama ya CCM itakutana kesho mjini Dodoma kuanza shughuli yake ya kupitia taarifa za wagombea 38 wanaoomba kuwania urais na kisha kuwasilisha ushauri wake kwenye kikao cha Kamati Kuu inayokutana keshokutwa. Habari kutoka ndani ya CCM zinasema kuwa kamati hiyo inayoongozwa na mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete wakati mwingine hukasimisha shughuli zake kwa kamati ndogo inayoketi chini ya Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Philip Mangula. Mangula amekaririwa mara kadhaa akisema chama hicho kitatumia vigezo 13 vilivyowekwa na chama kuwachuja wagombea hao, akisisitiza kuwa watateua mgombea mwadilifu, mwenye uzoefu na atakayeuzika kwa wananchi. Baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo walioko tayari mjini hapa kwa kazi hiyo walilieleza gazeti hili kuwa jukumu kubwa la kamati hiyo ni kuishauri Kamati Kuu juu ya masuala yote yanayohusu maadili ya wanachama na wagombea wa nafasi mbali ndani ya chama na kwenye vyombo vya Dola. Mjumbe mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini kwa kuwa si msemaji alieleza kuwa kama kuna jambo kubwa, kamati ndogo huwa haikutani, badala yake kamati kubwa ikiwa chini ya Rais ndiyo hukutana na kuandaa taarifa za kuwasilisha kwenye Kamati Kuu. Alitolea mfano wa mambo makubwa kuwa ni kama vile kupitia majina ya wanaowania kuteuliwa kugombea urais, kwamba kazi ya kamati ni kueleza taarifa za kila mwombaji, mazuri yake, mabaya yake na ushauri inaoutoa kwa wajumbe wa Kamati Kuu. Mjumbe huyo alisema, Kamati ya Maadili na Usalama haina mamlaka ya kukata au kuongeza majina ya wagombea na kwamba mambo yanayopelekwa kwenye Kamati Kuu ni yale mazito tu. Kuhusu mambo ya madogo yanayoishia kwenye kamati ndogo, alisema ni yale yanayoonekana yana viashiria vya majungu. Mangula hakupatikana jana kuzungumzia majukumu ya kamati hizo lakini Makamu mwenyekiti mstaafu wa CCM, Pius Msekwa alipoulizwa kwa simu alisema majukumu na mipaka ya Kamati ya Maadili na Usalama vimeelezwa ndani ya Katiba ya CCM. Hata hivyo, katika katiba ya CCM matoleo ya 2005 na 2010 kamati hiyo haikuonekana na mmoja wa wajumbe wa Kamati Kuu ambaye pia hakupenda kutaja jina lake, alisema haijatajwa kwenye kanuni za uchaguzi wala katiba ya CCM. Alisema badala yake mchakato wa kumteua mgombea urais kwa mujibu wa kanuni na katiba unaanzia kwenye Kamati Kuu ambayo hata hivyo, haiwezi kufanya kazi ya kutoa na kupokea fomu za wagombea urais, badala yake kamati kama hizo (za maadili) zikawepo kwa ajili ya kuisaidia Kamati Kuu. Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nauye alipotafutwa kutoa ufafanuzi juu ya suala hilo, alijibu kwa mkato kuwa yuko kwenye kikao. Wajumbe wa kamati Wajumbe wanaotajwa kuwamo kwenye Kamati ya Maadili na Usalama ni Mwenyekiti, Rais Jakaya Kikwete, Makamu wenyeviti, Philip Mangula (Bara) na Dk Ali Mohamed Shein (Zanzibar), Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana, Naibu makatibu wakuu, Vuai Ali Vuai (Zanzibar) na Rajabu Luhwavi (Bara), Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk Pindi Chana na Shamsi Vuai Nahodha. Wajumbe wa Kamati Ndogo ya Maadili na Usalama wanaotajwa ni Mangula ambaye ni mwenyekiti wa kamati hiyo. Wengine ni Kinana, Vuai, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, Katibu wa Sekretarieti ya Kamati Kuu, Anamringi Macha, Dk Maua Daftari, Shamsi Vuai Nahodha, Dk Chana na Mzee Masoud. Baada ya kazi ya wajumbe hao kukamilika taarifa itawasilishwa kwenye Kamati Kuu ambayo inaweza kuzitumia au kuziacha wakati wa kufanya mchujo na kupata wagombea wasiopungua watano watakaopelekwa kwenye Halmashauri Kuu ya Taifa Ijumaa. Halmashauri Kuu ya Taifa nayo itawachuja tena na kubakiza watatu watakaopelekwa kwenye Mkutano Mkuu wa Taifa Jumamosi na Jumapili ili kupata mgombea urais wa CCM. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Aficha Mwili wa Marehemu ndani kwa Siku sita bila watu kufahamu

$
0
0

Mama mmoja aliyejulikana kwa jina la Biti Karo Mkazi wa Mkuranga, Kimanzichana Mtaa wa Makonde amefanya tukio la ajabu na la kushanga kwa jamii, mara baada ya kukaa na mwili wa marehemu Mama yake kwa muda wa siku sita ndani bila hata ndugu na majirani zake kufahamu. Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kinasema Biti Karo alikuwa anakaa na Mama yake (Marehemu) akimuuguza. Biti Karo aliyehusika kuuficha Mwili wa Marehemu Chanzo chetu kinazidi kueleza kwamba, Majirani waliaanza kupata wasiwasi mara baada ya kutokumuona Mama huyo (Marehemu), kwani walikuwa wamemzoea akiwa nje na mwanae (Biti Karo) akiwa anampa dawa na chakula lakini ilipita siku kadhaa bila ya kumuona Mama huyo. Majirani wakiwa kwenye eneo lililotokea msiba Majirani walipoenda kumuulizia Biti Karo aliwajibu kwamba hajambo na yupo ndani amelala, lakini mnamo tarehe 4 july kijana mmoja alihisi harufu kali sana maeneo ya nyumba ya Biti Karo na alipojaribu kuuliza ni harufu ya nini, Biti Karo alijibu kwa kusema kwamba inawezekana ni harufu ya Panya. Mwili wa Marehemu ukionekana kwa mbali Mnamo siku ya jumapili july 5 Mama mmoja aliyejulikana kwa jina la Bibi Huruma ambaye ni ndugu wa Biti Karo alikwenda kuwatembelea na kumjulia hali mgonjwa, alipofika alishangaa kusikia harufu kali na alipouliza ni harufu ya kitu gani?, Biti Karo hakujibu kitu chochote. Bibi Huruma alipoingia ndani alikuta Mama yao amefariki huku mwili wake ukitoa harufu na sehemu nyingine zikiwa zimechanika na kupasuka ndipo hapo alipopiga mayowe na majirani kusogea eneo hilo. Majirani wote walishangaa kuona tukio hilo ambapo wengine walienda kumtaarifu Mjumbe aliyejulikana kwa jina la Kuisele, Mjumbe alimuita Mwenyekiti kisha wakawapigia simu Polisi. Baada ya Polisi kufika na kuchukua maelezo waliamuru mwili wa marehemu kuzikwa. Majirani wakiwa eneo la tukio Chanzo chetu cha habari kinanaeleza kwamba mwili wa marehemu ulikuwa umeharibika sana na ilikuwa ngumu hata kuoshwa hivyo ulizikwa bila ya kuoshwa na wala kufanyiwa heshima yoyote. Vijana wakiwa kwenye harakati ya kuchimba kaburi kwa ajili ya kuzika mwili wa Marehemu Baada ya mwili wa marehemu kuzikwa Polisi waliondoka huku wakiwaacha wakazi wa eneo hilo kwenye hali ya kutofahamu nini kinaendelea kwani mpaka sasa Biti Karo yupo huru na wala haonyeshi hali ya kustushwa kwa kile kilichotokea. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat


Pwani kuanza kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la kupiga kura

$
0
0

Zoezi la uandikishwaji kwenye daftari la kudumu la kupiga kura kwa njia ya kieletroniki BVR lipo mkoa wa Pwani kwa sasa na linaanza rasmi leo tarehe 7 mwezi wa saba. Zoezi hilo linatarajiwa kumalizika mnamo tarehe 20 ambapo uandikishwa utafanyika kwa awamu na makundi mawili. Mratibu Uchaguzi mkoa wa Pwani ndugu Shangwe Twamala ametoa ufafanuzi wa namna zoezi hilo litakavyofanyika ambapo amesema, awamu ya kwanza itafanyika kwa siku saba kisha baada ya hapo mashine zitahamishwa kwenda sehemu zilizosalia napo zoezi hilo litafanyika kwa siku saba. Pia Shangwe Twamala amewataka wakazi wa Mkoa wa Pwani kujitokeza kwa wingi ili kufaniksha zoezi hilo. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Iniesta: Haitowezekana Kwa Man Utd Kumsajili Ramos

$
0
0

Kiungo wa klabu bingwa nchini Hispania, Andres Iniesta amepingana na vyombo vya habari vya nchini England, vinavyoendelea kulikuza sakata la uhamisho wa beki wa klabu ya Real Madrid, Sergio Ramos. Iniesta amesema suala la kuondoka na Ramos nchini Hispania na kujiunga na klabu ya Man Utd kwake halipo na katu hawezi kulikubali kutokana na kuamini kwamba Los Blancos hawawezi kumuachia beki huyo. Amesema, Sergio Ramos ni beki anayetumainiwa kwa kiasi kikubwa katika klabu hiyo ya mjini Madrid na endapo atakubaliwa kuondoka, pengo lake haliwezi kuzibika kirahisi. Hata hivyo Iniesta amesema Man Utd ni klabu kubwa kama ilivyo Real Madrid, na inaweza kufanya lolote katika mipango ya usajili ya beki huyo mwenye umri wa miaka 29, lakini bado akaendelea kusisitiza kizingiti cha kubaki kwa Ramos kitaendelea kuwa viongozi wake. Ramos amekua akihusishwa na mipango ya kutaka kuhamia Old Trafford baada ya kuibuka mzozo kati yake na viongozi wa klabu ya Real Madrid unaohusu thamani ya mkataba wake mpya ambao bado hajausaini FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Steven Gerrard awafanyia Surprise Mashabiki wa Marekani

$
0
0

Hatimae aliyekua nahodha na kiungo wa klabu ya Liverpool, Steven George Gerrard amejitokeza hadharani na kuwasalimu mashabiki wa klabu ya LA Galaxy baada ya kuwa shuhuda wa mchezo wa klabu hiyo wa ligi ya nchini Marekani MLS mwishoni mwa juma lililopita. Gerrard ambaye ameitumikia klabu ya Liverpool kwa muda wa miaka 24 tangu akiwa na umri wa miaka 7, alikua katika fununu za muda mrefu za kuelekea nchini Marekani kucheza soka katika ligi ya nchini humo. Alionekana wakati wa mchezo wa MLS pale klabu yake mpya wa Los Angles Galaxy ilipua ikipambana na Toronto FC na kuibuka na ushindi wa mabao manne kwa moja. Gerrard anajiunga na mchezaji ambaye aliwahi kuchez akatika ligi ya nchini England katika klabu ya Tottenham Hotspurs Robbie Keane ambaye katika mchezo huo alifanikiwa kufunga mabao matatu. Mashabiki wa LA Galaxy wameonyesha kufurahishwa na kuridhishwa na kitendo cha iungo huyo mwenye umri wa miaka 35 kujitokeza mbele yao na kuwasalimu, ambapo sasa wanaamini kikosi chao kitaendelea kuimarika. Katika mtandao wa kijamii wa Twitter mashabiki wa LA Galaxy waliweka picha za mivinyo pamoja na makopo ya vilevi mbali mbali na kuzinakshia picha hizo kw amaneno yaliyosomeka Welcome Steven Gerrard. Hii itakua ni mara ya pili kwa klabu ay LA Galaxy kumsajili gwiji wa soka kutoka nchini Englad, baada ya kufanya hivyo miaka minane iliyopita kwa kumsajili David Robert Joseph Beckham mara baada ya kukamilisha mkataba wa kuitumikia klabu ya Real Madrid. Gerrard anaondoka Liverpool akiwa ameacha kumbu kumbu ya kucheza michezo 504 na kufunga mabao 120. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

De Gea kuanza mazoezi Manchester United

$
0
0

Mlinda mlango wa klabu ya Man Utd, David De Gea atakuwa sehemu ya wachezaji wa klabu hiyo watakaoanza mazoezi hii leo ya kujiwinda na msimu mpya wa ligi ya nchini England. De Gea anatarajiwa kuanza mazoezi na kikosi cha Man Utd ikiwa ni baada ya siku kadhaa kuonekana mjini Madrid ambapo uvumi uliendelea kudai kwamba mipango ya kutaka kujiunga na klabu ya Real Madrid ilikua inaelekea ukiongoni. Kati kati ya juma lililopita Meneja wa man Utd alimtaka kipa huyo chaguo la kwanza la Man utd kufika mazoezini bila kukosa mwanzoni mwa juma hili, hali ambayo itatimizwa hii leo. Hata hivyo kituo cha televisheni cha mjini Madrid kiitwacho Cuatro, kimeripoti kwamba pamoja na matarajio ba De Gea kuwa sehemu ya kikosi cha Man utd kitakachoanza mazoezi hii leo, bado viongozi wa Real Madrid hawajakata tama ya kumsajili katika kipindi hiki cha majira ta kiangazi. David De Gea amekua gumzo la kutaka kusajiliwa na klabu ya Real Madrid kwa kipindi kirefu, kufuatia mlinda mlango wa sasa wa klabu hiyo Iker Casillas Fernández kuonekana uwezo wake unazidi kuporomoka siku hadi siku. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

LIPUMBA: Tutaitisha Maandamano Mikoa Yote Yenye GESI

$
0
0

Chama cha Wananchi (CUF), kimesema kitaitisha maandamano kwenye mikoa yenye gesi ili kulishinikiza Bunge kupinga muswada wa mafuta na gesi uliopitishwa juzi. Akihutubia wakazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji na viunga vyake, Mwenyekiti wa Taifa wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, alisema haoni mantiki na hakuna sababu ya kufanya haraka kupitisha muswada huo. “Suala hili linahitaji mjadala wa kina utaohusisha wadau mbali mbali, wataalamu na wananchi kwa ujumla wake,” alisema Profesa Lipumba na kuongeza: “CUF inaunga mkono jitihada za wabunge wa kambi ya upinzani kwa hatua zao kupinga muswada huo, ambao haukujali na wala haukuzingatia maslahi ya Taifa.” Alisema CUF inatoa angalizo kwa Rais Jakaya Kikwete kwamba kwa hali inavyoenda huenda akaenda kufunga Bunge litalokuwa na Wabunge wa CCM pekee. “Hiyo inatokana na ukweli kwamba Spika wa Bunge amepoteza muelekeo na ameshindwa kabisa kuliongoza Bunge kwa mujibu wa kanuni walizojiwekea katika kutimiza wajibu,” alisema Profesa Lipumba na kuongeza: “Kwa hiyo  basi, Rais Kikwete atakuwa amefuata nyayo za Rais wa Zanzibar.” Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein Juni 26, mwaka huu alilivunja Baraza la Wawakilishi bila Wawakilishi wa CUF kuwapo barazani. Wajumbe hao walisusia Baraza hilo kutokana na kutoridhishwa na uandikishaji wa wapigakura katima daftari la kudumu la wapigakura kwa kutumia mfumo wa kielektroniki unaojulikana kama Biometric Voters Registrarion (BVR), wakisema kuwa uandikishaji huo ulitawaliwa na ubabe. Profesa Lipumba alionya kuwa kama Bunge litaendelea na mpango wake huo, basi CUF  itaitisha maandamano ili kupinga muswada huo. Katika hatua nyingine, Profesa Lipumba alisema kuwa Mkoa wa Kigoma unaweza kuendelea kiuchumi ikiwa utatumia vizuri rasilimali zilizoko akitolea mfano Hifadhi ya Taifa ya Gombe kwamba ikitumika vizuri inaweza kuingiza mapato mengi. Alisema kwamba jiografia ya Mkoa wa Kigoma inauruhusu kupata fursa nyingi za kuendelea kiuchumi kwa kuwa wananchi wake wanaweza kufanya biashara na nchi zinazouzunguka za Burundi Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Viewing all 553 articles
Browse latest View live